KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 31, 2014

Taifa Stars yawasili Johannesburg kabla ya kuelekea Maputo hapo kesho

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama jana (Julai 30 mwaka huu) hapa Johannesburg kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kwenda Maputo, Msumbiji kwa ajili ya mechi dhidi ya Mambas itakayochezwa Jumapili.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi mara mbili leo- asubuhi na jioni kwenye uwanja wa Bedfordview Country Club. Mazoezi ya mwisho yatafanyika kesho asubuhi (Agosti 1 mwaka huu) kabla ya baadaye jioni kuanza safari ya Maputo.
 Wakati huo huo, Balozi wa Tanzania hapa Afrika Kusini, Razia Msuya baadaye leo jioni atazitembelea timu zote mbili za Tanzania zilizopo hapa Johannesburg kusalimia wachezaji.
Serengeti Boys yenyewe ipo hapa tangu Julai 27 kwa ajili ya mechi dhidi ya Afrika Kusini itakayochezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu).