KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 30, 2014

Wazimu wa soka waingia Marekani: Mchezo wa Real Madrid dhidi ya Manchester United Jumamosi Marekani kuvunja rekodi ya dunia ya watazamaji

Nguvu ya mashabiki: Ikitokea katika ligi kubwa kabisa ya Premier League Manchester United imekuwa ikifuatiliwa na wengi nchini Marekani
Mchezo wa kirafiki baina ya Manchester United dhidi ya Real Madrid unatazamiwa kuhudhuriwa ma watazamaji takribani 109,000 mjini Detroit mchezo ambao utapigwa Jumamosi.
Vigogo hao wa Ulaya watacheza mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi wa michuano ya 'International Champions Cup' uwanja wa Michigan huko Ann Arbor.
Manchester United iliyo chini ya Louis van Gaal inaonekana kuwa moto katika michuano hiyo na inaangaliwa kuwa ianweza kusonga mbele na kucheza fainali ya ligi hiyo ya michezo ya kirafiki endapo watawafunga mabingwa hao wa Ulaya katika ardhi ya Marekani.

Sell out: Manchester United's match against Real Madrid will be watched by 109,000 fans
Mchezo wa Manchester United dhidi ya Real Madrid utahudhuriwa na takribani mashabiki 109,000
Global superstars: Wayne Rooney and Cristiano Ronaldo could both feature at the Michigan Stadium in Detroit
Nyota wa dunia: Wayne Rooney na Cristiano Ronaldo huenda wote wataonekana uwanjani uwanja wa Michigan huko Detroit

Wote Manchester United na Real Madrid wanaonekana kuwa na mashabiki wengi wakijenga himaya kubwa ya wapenzi wao huko Marekani kwa kuweka maandalizi yao kabla ya msimu mpya nchini huko.
Manchester United ilicheza na Inter Milan JUmanne usiku ambapo mashetani wekundu walishinda kwa penati ambapo takribani mashabiki 61,238 waliushuhudia huko FedExField.
Kama ilivyo kwa Wayne Rooney, Cristiano Ronaldo naye Gareth Bale anatarajiwa kuwemo kikosini hiyo Jumamosi ambao utaonyesha ni kwa kiasi gani mashabiki wa soka Marekani wameanza kuwa wendawazimu wa soka kufuatia kununuliwa kwa wingi kwa tiketi za mchezo huo.

Linganisha mahudhurio ya michezo mingine na matukio mengine yaliyopita viwanjani na mchezo wa Jumamosi

Super Bowl XLV - 103,219
London 2012 Olympics (100m final event) - 80,000
2014 World Cup final - 74,738
2014 Open Championship at Hoylake (July 18) - 43,183
Wimbledon final matches scheduled on Centre Court - 15,000