Maximo akitoa vitu kwa mshambuliaji Jerson Tegete |
KAGAME CUP RWANDA
Kocha mkuu wa Dar es salaam Young Africans Marcio Maximo
amesema klabu yake inasubiri barua maalum kutoka baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika mashariki na kati CECAFA na kujua nini cha kufanya.
Maximo ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika muda mfupi baada ya mazoezi uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola iliyoko Mabibo jijini Dar es Salaam.
Maximo ambaye anaonekana kukiamini mno kikosi chake kwa sasa amesema anasubiri kauli ya CECAFA kupitia kwa viongozi wake na kwamba kikosi chake kipo vizuri.
Maximo amesema taarifa ambazo amezipata mpaka mapema hii leo
asubuhi ni kwamba viongozi wa baraza la vyama vya soka afrika mashariki na kati
CECAFA bado hawajaiarifu klabu ya Dar es salaam Young Africans juu ya ushiriki
wa michuano ya mwaka huu.
Amesema endapo barua ya kuarifiwa kwa Dar es salaam Young
Africans kutoka CECAFA itawasili hata tesho asubuhi na akapewa ruhusana
kuondoka na kikosi chake kwenda Kigali Rwanda, hatosita kufanya hivyo kutokana
na kuhitaji michezo ya ushindani kwa ajili ya kujiwinda na msimu mpya wa ligi.
Katika hatua nyingine
Kwa upande wa maandalizi ya kikosi, Maximo amesema kikosi
chake kinaendelea vyema na mazoezi ya kila siku kwenye uwanja wa shule ya
sekondari ya Loyola jijini Dar es salaam.
Amesema mbali na mazoezi pia amekuwa akiwahusia wachezaji
wake suyala la kujituma na kuweka mbele uzalendo wa kuitumikia Dar es salaam
young Africans ambayo inahitaji kutoka hapa ilipo na kwenda mbele zaidi.
Amesema kwake yeye mchezaji mwenye nafasi ni yule anayejituma na kujitoa kwa timu na si mchezaji mbinafsi.
No comments:
Post a Comment