Kikosi cha Kenya katika mashindao ya Jumuiya ya madola, yanayoendelea
mjini Glascow, kinakabiliwa na wakati mgumu, kutoka na matatizo kadhaa.
Sasa imebainika kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya hawana vifaa vya michezo.
Naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya Tecla Lorupe
amesema kuwa wao walifahamishwa siku ya Alhamisi kuwa baada ya
wanariadha hawajapokea vifaa na sare zao za michezo.
Lorupe ambaye, ni bingwa wa zamani wa dunia
katika mbio za masafa marefu za Marathon, amesema wao wameshangazwa sana
na tukio hilo.
Amesema kumekuwa na matatizo ya kuwasilisha vifaa hivyo vya wanamichezo wa Kenya, kutoka kwa kampuni inayotengeneza mavazi hayo.
Aidha amesema nusura mabondi wa Kenya wakose kushiriki katika mashindano ya mwaka huu, kutokana na ukosefu wa vifaa vyao.
Lorupe amesema walipata bahati wakati, kamishna
wa michezo nchini Kenya Gordon Oluoch alipolazimika kutumia fedha fedha
zake kununua vifaa hivyo ambavyo vilitumika na mabondia siku ya Ijumaa.
Siku ya Alhamisi, muogeleaji wa Kenya Jason
Dunford aliondolewa katika shindano ya mita hamsini butterfly, kutokana
na kile alichokitaja kama kutopata vifaa kwa wakati unaofaa.
Mbali na wanariadha kukosa vifaa na mavazi yao,
wasimamizi wa michezo mbali mbali nao wanalalamika kuwa hawajapata
marupurupu yao.
Tecla Lorupe |
Hali hii imelleta wasi wasi katika kambi ya kenya huku baadhi ya wanariadha wakiondolewa mapema katika mashindano ya mwaka huu.
Baadhi yao wanasema, hali duni katika kambi ya maandalizi na hapa mjini Scotland huenda ikaadhiri matokeo ya timu ya Kenya.
No comments:
Post a Comment