Michuano ya jumuia ya Madola kwa mwaka 2014, imefunguliwa rasmi hii leo jijini Glasgow nchini Scotland huku mataifa 71 yakitarajiwa kushindana katika michezo 17 tofauti, ambayo itaanza kutimua vumbi lake kesho.
Tayari waziri mkuu wa nchini Scotland, Alex Salmond ameshathibitisha
kukamilika kwa maandalizi ya michuano hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu
kubwa na wadau wa michezo duniani kote, huku kila nchi ikiamini wawakilishi wao
wataibuka na medali ima za dhahabu, shaba ama fedha.
Salmond amewataka wachezaji kutoka kila kona ya dunia
kujihisi wapo nyumbani na washiriki michuano hiyo kwa amani ambayo itafikia
tamati August 3.
Hata hivyo kiongozi huyo amewasihi wanamichezo
watakaoshiriki michuano ya Jumuia ya Madola kwa mwaka huu huko mjini Glasgow,
kujiepusha na kadhia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni, ili kuepuka
balaa ambalo huenda likawaharibia maisha yao ya baadae katika nyanja ya
kimichezo.
Amesema vipo vinywaji vya kawaida ambavyo vinatumika na
vinaruhusiwa kwa wanamichezo kuvitumia wakati wote, lakini wasithubutu kwenda
nje ya maadili kwa kunywa vinywaji ama dawa zenye chembe chembe za kuongeza
nguvu.
Waziri mkuu wa nchini Scotland, Alex Salmond. |
No comments:
Post a Comment