Arsenal imekubali mpango wenye gharama ya pauni milioni £12 kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa pembeni wa Newcastle United
Mathieu Debuchy na inatarajiwa kutangaza uhamisho wake baada ya fainali ya kombe la dunia.
Taarifa za Debuchy kuhusishwa na Arsenal zilichochewa zaidi na vyombo vya habari wiki iliyopita ambapo meneja wa Arsenal aliripotiwa kuweka mpango huo katika nafasi ya juu kwa lengo la kupata mlinzi atakayeziba pengo la Bacary Sagna.
Taarifa za uhakika ambazo pia zimeripotiwa katika gazeti la Daily Star zinasema kuwa pauni milioni £12 imekubaliwa na kwamba mchezaji huyo atathibitishwa rasmi na klabu hiyo baada ya fainali ya kombe la dunia.
Akiwa na umri wa miaka 28 mlinzi huyo kwasasa ana majukumu mazito katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kianchojipanga kwa ajili ya hatua ya robo fainbali ya michuano ya kombe la dunia na huenda Ufaransa ikarejea nyumbani mwishoni mwa juma kama watapoteza mchezo wao dhidi ya Ujerumani Ijumaa usiku.
Mwenyewe Debuchy, aliripotiwa wiki iliyopita akisema kutaka timu ambayo ina nafasi ya kucheza michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya ambapo huko nyuma alihusishwa na vilabu vikubwa vya PSG
na Real Madrid.
No comments:
Post a Comment