KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 2, 2014

Nyota kumi ambao hukuwajua hapo kabla ambao sasa klabu yako uipendayo inaweza kuwasajili kiangazi

Islam Slimani – Algeria
Mshambuliaji huyo ni mwepesi na ni mwenye nguvu, Slimani alifunga magoli mawili katika kombe la dunia na amevutia sana kutokana na kujituma na uwezo wake . Mmaliziaji mzuri na huenda akaihama Sporting Lisbon endapo kutapatikana mazungumzo ya kuelewana na vilabu vingine wakati huu wa usajili wa kiangazi

Ricardo Rodriguez – Switzerland
Rodriguez yuko vizuri akiwa na umri wa miaka 21 lakini ameweza kuonyesha uwezo na uzoefu wake nchini Brazil. Mwepesi na mpigazi mzuri wa krosi ana uwezo kukimbia kwa kasi upande wa ulinzi wa kushoto na kupiga krosi akiwa na uwezo mkubwa. Kwasasa anaichezea Wolfsburg ya nchini Ujerumani.

Divock Origi – Belgium
Alikuwa ni chaguo la kushangaza katika kikosi cha kwanza cha Ubelgiji lakini alifunga goli muhimu katika mchezo muhimu dhidi ya Russia ambapo alionyesha mengi ya kutumainia. Ana nguvu , kasi na mwenye kulitazama goli, tayari Liverpool wana mnyemelea mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 19.


Kostas Manolas - Greece
Mipango ya uchezaji ya kikosi cha Ugiriki ilikuwa inaanzia nyuma sehemu ya ulinzi ambako Manolas alikuwa ndio mpango mzima. Akiwa na umri wa miaka 21 mlinzi huyu alikuwa akionyesha wazi kuwa ni kiongozi katika kupanga safu ya ulinzi.  Ana nguvu na ana kuwa bora anapokuwa hewani, huenda klabu yake ya Olympiacos ikamkosa.

Kaylor Navas – Costa Rica
Mlinda mlango ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika kikosi cha Levante, lakini pia ameudhihirishia ulimwengu kuwa ni kifaa hususani katika msimu huu wa fainali za kombe la dunia nchini Brazil akiwa na timu ya taifa ya Costa Rica. Mdakaji wa mashuti makubwa ambaye uwepo wake umeonyesha umuhimu kikosini. Makipa kama yeye ni mara chache kutokezea.

Memphis Depay – Holland
Kulikuwepo na minong'ono mingi ya wasiwasi nchini Uholanzi juu ya kinda huyu, lakini Depay amedhihirisha kipaji chake duniani katika fainali hizi za kombe la Dunia. Ni winga tereza ni ujuzi na akili, ameonyesha uzuri wake kikosini Uholanzi. atakuwa wa gharama lakini ni nyota wa ukweli katika kutengeneza.


Rais M’Bolhi – Algeria
Mlinda mlango huyu wa Aljeria M’Bohli anaonekana kama hatimaye atapata uhamisho mnono kiangazi kama wenye macho mazuri walifanikiwa kumuona. Alionyesha kuokoa michomo kadhaa iliyoelekezwa katika upande wake.

Miguel Layun – Mexico
Layun alikuwa katika miezi 12 ya ubora lakini zaidi ameng'ara katika kombe la dunia nchini Brazil. Mlinzi wa kushoto ambaye ana weza pia kucheza eneo la ulinzi wa nyuma wa kulia, anajua namna kupanda kutoka nyuma pia anafunga. Anachezea Club America ya Mexico.

Shkodran Mustafi – Germany
Baada ya kuwepo kwa muda mfupi katika klabu ya Everton ya England sasa ameelekea nchini Italia. Ana umri wa miaka 22 tu lakini anaonekana kuwa atakuwa mwiba baadaye katika siku za usoni. An mwili mkubwa, ana nguvu, mlinzi wa kati mwenye kimo kirefu ambaye aliziba pengo la ulinzi wa kulia katika kikosi cha Ujerumani katika kombe la dunia

Charles Aranguiz – Chile
Aranguiz alifunga pengine penati nzuri zaidi kwa Chile walipokutana na Brazil mchezo wa hatua ya mtoano ya 16 bora ambao uliamuliwa kwa mikwaju ya penati, alionyesha uwezo wa kiufundi. Kiungo mwenye uwezo wa kuchezea mpira huku akifungua macho kutafuta wapi kwa kuupeleka mpira, ana umri wa miaka 25 lakini bado ana vitu vingi vya kuongeza ujuzi wake.
Fabian Johnson – USA
Ameshapata timu mpya kiangazi hii, kwa kweli  Johnson alikuwa na kiwango kizuri cha kuvutia. Ni hivi karibuni tu atakuwa katika uhamisho mwingine licha ya kuwa amesajili kiangazi.  Anajituma, ana kasi na anafanya yote akiwa mchezo kuzuia na kushambulia akitokea pembeni.Ni mchezaji wa kuvutia sana.

Guillermo Ochoa – Mexico
Kwasasa yuko huru, ni inawezeakana simu ya Ochoa ikawa inaita mara zote baada ya kiwango cha juu katika kikosi cha  Mexico. Aliokoa michomo kadha na bila shaka atakuwa katika mazungumzo hivi sasa. Hakujulikana kabla ya kombe la dunia lakini sasa anajua kuwa kila mtu ana mtaka.

No comments:

Post a Comment