Kikosi cha Serengeti Boys |
Msafara wa watu 25 wa kikosi cha
timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) unaondoka
kesho (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi dhidi ya
Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi
ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville
uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika
Kusini.
Timu hizo zilitoka suluhu katika
mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex
uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya mwisho ya michuano
hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri na Congo Brazzaville.
Fainali za Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.
Wachezaji wanaounda kikosi cha
Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege ya Fastjet
ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo, Abutwalibu Hamidu Msheri,
Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi, Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias
Mdamu.
Wengine ni Badru Haji Othman,
Baraka Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus
Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa Abdallah,
Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce Mushin na Seif Said Seif.
Benchi la Ufundi linaongozwa na
Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall (Mshauri wa
Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba (Daktari), na Edward
Venance (Mtunza vifaa).
Msafara wa timu hiyo itakayorejea
nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid Mohamed Abdallah.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment