Kikosi cha Stars |
Timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imejiweka katika mazingira magumu ya
kufuzu kwa hatua ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika(AFCON),
fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Morroco.
Ikiwa
katika uwanja wake wa nyumbani wa Taifa, mbele ya maelfu ya mashabiki
wake aliokuwa nyuma yao, Stars imelazimishwa sare ya bao 2-2, ambapo
sasa watalazimika kushinda au kupata sare ya kuanzia mabao 3-3 ugenini
katika mchezo wa marudiano utakaopigwa Agosti 1 na 3 mwaka
huu nchini Msumbiji.
Stars
ilikuwa imesheheni wachezaji wake wote muhimu akiwemo kiungo Mwinyi
Kazimoto, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na mlinzi kitasa Shomari
Kapombe ambapo imeonekana dhahiri kuwa inahitaji mbinu mpya ya kuweza
kufanya ulinzi wa kipolisi inapokuwa inashambulia ili kuzuia madhara
langoni mwao. Golini alikuwa Deogratius Munish Dida ambaye kutokana na
umakini mdogo wa walinzi wake waliokuwa wakiongozwa na nahodha Nadir
Haroub Canavaro walijikuta wakifungwa bao la pili kizembe muda mfupi
baada ya shambulizi zuri la Thomas Ulimwengu.
Mabao ya Stars yametiwa kwenye kamba na kiungo Khamis Mcha maarufu kama ‘Vialli’ aliyeingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa. Viali alifunga mabao hayo katika dakika za 65 na bao la pili dakika ya 71 kwa njia ya penati.
Mabao ya Msumbiji yamefungwa na Elias Pelembe na Isaack Carvalho aliyeingia kipindi cha pili. |

Mabao ya Msumbiji yamefungwa na Elias Pelembe na Isaack Carvalho aliyeingia kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment