Jaja akipokea nakala ya mkataba wake kutoka kwa Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu leo maraa baada ya kusaini kuitumikia kwa miaka miwili |
Mshamabuliaji Geilson Santos Santana "Jaja" raia wa
Brazil leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2014-2016) kuitumikia timu
ya Young Africans kwa ajili ya kuitumikia klabu kwa michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu
ya soka Tanzania Bara pamoja na mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika
mwakani.
Katibu mkuu wa Young Africans Beno Njovu amesema
usajli wa Jaja unakua ni wa pili msimu huu kwa wachezaji wa kimataifa
baada ya awali kumsajili kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho ambaye pia
ni raia wa Brazil.
"Kazi yetu uongozi ni
kutekeleza maelekezo ya kocha mkuu pamoja na benchi la ufundi, walitoa
mapendekezo ya usajili kabla hawajaanza kazi na mengine baada kuwasili
yote tunajitahidi kuyatekeleza ili kila kitu kiende safi" alisema Beno.
Jaja
ambaye alizaliwa tarehe 21 Septemba 1985 na kukulia katika mji wa
Aracaju nchini Brazili mpaka anasajiliwa na timu ya Young Africans
alikuwa akiichezea timu ya Itabaina FC iliyopo nchini Brazil.
Mshambuliaji
huyo mwenye mwili uliojaa vizuri tayari alishaanza mazoezi tangu
katikati ya wiki iliyopita chini ya Kocha Mkuu Marcio Maximo na msaidizi
wake Leonado Neiva ambao wanaendelea kukinoa kikosi cha Young Africans
kwa ajili ya michuano mbalimbali.
No comments:
Post a Comment