KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 17, 2014

YUSUFU MANJI AWAAMBIA WANA YANGA KUWA UONGOZI WAKE KAMWE HAUTA MUINGILIA KIKAZI KOCHA MAXIMO

Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji

Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Young Africans Yusuph Mehboub Manji amesema katu uongozi wa klabu hiyo hautomuingilia kocha mkuu  Márcio Máximo Barcellos ambaye anaendelea kukisuka kikosi chake kwa kufanya usajili wa wachezaji kutoka nje ya nchi.
Manji amesema kinachofanywa na kocha huyo kutoka nchini Brazil wanakiafiki kwa asilimia mia moja na uongozi utafuata maelekezo yake pale itakapohitajika.
Mpaka sasa klabu ya Dar es salaam Young Africans imeshavuka hitaji la kuwa na wachezaji watano wa kimataifa baada ya kuwasili kwa mshambuliaji kutoka nchini Brazil Geilson Santana Jaja.
Wachezaji waliokuwepo kabla ya kuwasili kwa mshambuliaji huyo ni Emmanuel Okwi, Khamis Kiiza Diego, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite pamoja na Andrey Coutinho

SAUTI YA YUSUFU MANJI