KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, August 2, 2010

KAMA HUMJUI MJINI ANAKUPOTEZA KWASABABU YA UBISHI WA TOWN

Alisoma Jitegemee Enzi zile ikiitwa “jiteute “akaelekea mbeya na kurejea Dar na kuanza kazi ya usanii, kapita kwingi siwezi kumaliza kumuhadithia na kafanya kazi nyingi na ndiyo maana anajiita mbishi wa wa-town kama unabisha sasa jifanye wewe wa mjini kuliko yeye uone kazi yake.
Binafsi nimemjua tangu Meta sekondari na baadaye kama mtangazaji wa Times Fm,redio free Afrika,Triple A Arusha na sasa Uhuru Fm duh! Jamaa mbishi kwenye microphone sit u kutangaza mpaka kuimba yaani jamaa anaijua microphone si kitoto kotekote ni MC mwenye kucheza kotekote kama ni mchezaji wa soka basi jamaa namba zote, unajua nani huyo hapo juu sasa njema na ndio maana anakutishia mkwanja japo madafu ingekuwa dolari ingekuwaje.
Anaitwa Anslem Triphone Ngaiza a.k.a SOGGY DOGY HUNTER siku hizi tunamwita Sogy kifupi maana muda hautoshi kumaliza majina yote. Kutana naye uhuru FM kila siku za wiki kuanzia saa nane mpaka saa kumi katika UHURU FLAVER kiwa na ndugu yake DR K katika machine usimsahau bi shosti Samira kiango “the great” .kipindi bomba ile mbaya ngoma za kijanja ambacho kinasikilizwa na wajanja hata kama uko kijijini wewe ni mjanja sikiliza kila siku jumatatu mpaka ijumaa don’t miss it.mi mbishi wa town wewe je.na wewe bisha ki-town tufanane.

No comments:

Post a Comment