"Kocha mpya wa timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Pablo Ignacio Velez kutoka Argentina wa kwanza kulia, akizungumza juu ya nini atafanya akiwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao uliopangwa kuanza Septemba Mosi mwaka huu. Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo. Wengine katika picha ni Charles Otieno ambaye ni mkurugenzi wa ufundi na Biashara wa timu hiyo na Meneja Mkuu na Mmiliki wa timu hiyo, Rahim Kangezi. Picha na Mpiga picha wetu".
Klabu ya African Lyon
leo hii imemtambulisha kocha wake mpya anayeitwa Pablo Ignacio Veles kutoka nchini Argentina ambaye Lyon inaamini kuwa ataisaidia timu hiyo na kuwapa mafanikio makubwa pale alipoachia mtangulizi wake
Charles Zamunda Kengezi .
Akionge na waandishi wa habari kocha huyo amesema ndoto yake
ilikuwa ni kuja barani Afrika na kufanya kazi ya kufundisha soka jambo ambalo amesema amefurahia kupata nafasi hiyo katika timu ya Afrika Lyon kwa kuwa
ametimiza ndoto yake na amekuja Afrika
si kusaka pesa bali kujitolea na kuendeleza mpira barani Afrika
Kocha huyo ameomba muda wa kutengeneza kikosi
kwani mchezaji lazima atengenezwe physically, discipline na uwezo wa kupiga
pasi ili aweze kuwa kuwa mchezaji kamili.
Katika
historia yake amesema hajawahi kuichezea timu kubwa isipokuwa amechezea vikosi
vya vijana vya under 17 na 20
Afrikan Lyon
imeingia naye mkataba wa miaka mitatu akiwa tayari ana program ya mwaka mmoja ya kufundishia.
Pablo anajua
kuongea lugha moja ya kireno tu jambo ambalo uongozi wa klabu hiyo umesema
kuwa hilo kwao si tatizo kwa kuwa
mkurugenzi wa ufundi wa klabu anajua vizuri lugha hiyo.
No comments:
Post a Comment