Kamati
ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA) imetangaza
kipindi cha pingamizi kwa waombaji uongozi katika uchaguzi wa chama
hicho utakaofanyika mwezi ujao.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ombeni Zavala, kipindi cha
pingamizi ni kuanzia Oktoba 5 hadi 9 mwaka huu, na pingamizi
ziwasilishwe ofisi za TWFA. Mwisho wa kupokea pingamizi ni saa 10 kamili
jioni, na hakuna ada kwa ajili ya pingamizi.
Pia
amesema usaili kwa wagombea utafanyika kati ya Oktoba 12 na 14 mwaka
huu kuanzia saa 3 asubuhi kwenye ofisi za TWFA zilizopo Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Kila mgombea anatakiwa kufika
kwenye usaili akiwa na vyeti vyake halisi (original) vya kitaaluma.
Waombaji
wa uongozi kwenye uchaguzi huo ni Lina Paul Kessy, Isabellah Hussein
Kapera na Joan Ndaambuyo Minja (Mwenyekiti) wakati mwombaji wa nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ni Roseleen Kissiwa.
Nafasi
ya Katibu Mkuu imevutia wagombea wawili; Amina Ali Karuma na Cecilia
Oreste Makafu. Mark Raghton Mhango ni mgombea pekee wa nafasi ya Katibu
Msaidizi kama ilivyo kwa Rose Msamila anayewania nafasi ya Mhazini.
Wagombea
wanne wameomba nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF). Wagombea hao ni Furaha Emily Francis, Zena
Suleiman Chande, Jasmin Badar Soud, Juliet Edwin Mndeme. Wanaowania
ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Rahim Salum Maguza, Triphonia Ludovick
Temba na Sophia James Charles.
No comments:
Post a Comment