Michuano ya ligi ya Uropa ilienndelea hapo jana,
katika kundi K Tottenham ya uingereza iliivuta chini Anzhi Makhachkala
ya urusi huko Moscow kwa mabao mawili kwa bila.
Katika Mechi nyingine
Swansea ya uingereza iliishinda St Gallen ya uswizi kwa bao moja kwa
bila na kuchukua uongozi katika kundi A
Wakati huo huo kocha wa timu ya taifa ya
Uingereza Roy Hodgson ameendelea kusisitiza kuwa lije jua ama mvua, kipa wake nambari
moja ni Joe Hart.
Mlinda lango huyo wa Man City alilaumiwa na wakosoaji
wengi katika mechi ya Jumatano dhidi ya Bayern Munich wakisema kuwa
uzembe wake ulichangia kwa kiasi kikubwa kuifanya timu yao kuwa taabani mikononi mwa Beyern iliyoicharaza mabao matatu kwa moja katika
michuano ya klabu bingwa ulaya.
Wakati Mashabiki wa Man City wakiuma vidole vyao
kuhusu utendaji kazi wa kipa wao, wapo baadhi ya Mashabiki wa Man U nao
wanaosema kocha David Moyes ameshindwa kazi lakini wamekumbushwa na
mtangulizi wake Sir Alex Fergeson kuwa Moyes anatosha.
Ikiwa hilo ni
kweli au la itajulikana, viwanjani ila kwa sasa Man U inashikilia nafasi
ya kumi na mbili katika msimamo wa ligii ya Uingereza jambo ambao
limewaacha wengi kujiuliza hatima ya Man U wanaotetea taji hilo.
No comments:
Post a Comment