KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, May 14, 2014

Rwanda yamtaka Stephen Constantine kuinoa Amavubi

Constantine anatazamiwa kufanya mazungumzo na shirikisho hilo la Ferwafa Alhamisi.
Timu taifa ya soka ya Rwanda inamtaka Raia Muingereza Stephen Constantine kuwa mkufunzi wake katika mkataba wa miaka miwili.
Tayari shirikisho la soka nchini humo limempendekezea mkataba wa miaka miwili.
Shirikisho la kandanda la taifa hilo linamtaka mkufunzi atakayechukua usukani baada ya Eric Nshiyamana, ambaye mkataba wake na timu hiyo utatamatika tarehe 31 mwezi Julai.
Kocha huyo wa zamani wa Millwall mwenye umri wa miaka 51, ana uzoefu wa kandanda ya bara la Afrika, hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Malawi tangia mwezi Februari mwaka wa 2007 hadi Aprili mwaka wa 2008.
Constantine anatazamiwa kufanya mazungumzo na shirikisho hilo la Ferwafa Alhamisi.
Msemaji wa Shirikisho la Soka la Rwanda bwana Vedaste Kayiranga aliiambia BBC kwamba makubaliano yalikuwa yamefikiwa.
Kocha wa zamani wa Ghana Ratomir Djukovic, kocha wa Botwana Peter Butler na kocha wa zamani wa Tanzania Kim Poulsen walikuwa miongoni mwa waliotarajia kupewa kazi hiyo lakini Kayiranga alisema kuwa walipendezwa na Constantine, na kwamba alikuwa tayari kujiunga na timu hiyo ya taifa la Rwanda.
Constantine aliye na leseni kutoka kwenye shirikisho la soka ulimwenguni majuzi aliisaidia Nea Salamis kutoka katika ligi ndogo ya Cypriot kufuzu kucheza katika ligi kuu. Constantine aliwahi pia kuwa mkufunzi wa mataifa ya Nepal, India, Malawi na Sudan.
Ferwafa inatarajia kukamilisha mipango hiyo wikendi hii nchini Tunisia wakati ambapo timu ya Taifa ya Rwanda itakuwa ikichuana na timu ya taifa ya Libya katika michuano ya kufuzu kwa mechi za mabingwa wa Afrika zitakazochezwa 2015. Kocha msaidizi bwana Cassa Andre Mbungo anatarajiwa kuiongoza timu hiyo wakati wa mchuano huo.
Ripoti katika wavuti wa Ferwafa zinaongezea kuwa kuna machache ambayo wanpaswa kuzungumzwa na Constantine kabla ya kumtangaza rasmi kama mkufunzi.

No comments:

Post a Comment