KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, May 14, 2014

Siku chache kuelekea kombe la dunia Scolari avurugwa kwa kukwepa kulipa kodi

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari,anatarajiwa kuchunguzwa na polisi kulingana na taarifa kutoka ncini Portugal licha ya kocha huyo kukanusha madai kuwa alikwepa kulipa kodi.
Bwana Scolari alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Portugal kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2008. Madai hayo yanaonekana kuhusishwa na wakati wake alipokuwa nchini humo.
Katika taarifa yake bwana Scolari alisema kuwa daima amekuwa akiweka wazi mapato yake kwa idara ya utozaji ushuru katika nchi zote alikofanya kazi.
Madai hayo yanakuja mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa kombe la dunia nchini Brazil.
Mwanasheria mkuu nchini Portugal amethibitisha taarifa za kuchunguzwa kwa Scolari, ingawa hakutoa taarifa zozote.
''Ninajiamini mimi mwenyewe sijafanya uhalifu wowote na nimekuwa nikitangaza mapato yangu. Ikiwa kuna jambo lolote ambalo haliko sawa , sio makosa yangu,'' alisema Scolari.

No comments:

Post a Comment