Mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baina ya wenyeji Mgambo JKT ya Tanga dhidi ya Mbeya City ya Mbeya umeshindwa kufanyika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jijini Tanga hii leo.
Mchezo huo uliokuwa usimamiwe na mwamuzi Izrael Mujinu Nkongo sasa utafanyika kwa mujibu wa kanuni hapo kesho endapo hali ya hewa itakuwa imetulia jijini humo.
Kwa mujibu wa msimamizi wa mchezo huo mwamuzi mstaafu Hamisi Kisiwa mara baada ya ukaguzi kufanywa na waamuzi wa mchezo huo iliamuriwa mchezo huo kusogezwa mbele kwa saa 24 kwa mujibu wa kanuni huku taarifa zaidi ikisubiriwa kutoka kwa wasimamizi wa ligi hiyo bodi ya ligi.
No comments:
Post a Comment