KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, August 28, 2010

ATLETICO MADRID YATWAA EUROPEAN SUPER CUP NDOTO ZA BERNITEZ KUTWAA TAJI LA PILI AKIWA NA INTER MILAN ZAYEYUKAAtletico Madrid imefanikiwa kutwaa taji la European Super Cup baada ya ushindi maridhawa wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa vilabu ulaya Inter Milan.
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Jose Antonio Reyes ndiye aliyekuwa wakwanza kuipa bao la kuongoza Atletico huko katika jiji la Monaco kwa shuti hafifu ambalo lilimpita mlinda mlango wa Inter Julio Cesar karibu na upande wake wa goli alikokuwa hiyo ikiwa ni dakika ya 62 ya mchezo

Karibu na kuelekea kukamilika kwa mchezo Simao Sabrosa alifanya kazi nzuri ya kutengeneza pande kwa Sergio Aguero na kuandika bao la pili.

Inter walifanikiwa penati katika dakika ya mwisho ya mchezo baada ya Raul Garcia kumfanyia madhambi Goran Pandev lakini hata hivyo mlinda mlango wa Atletico David de Gea alifanikiwa kuokoa penati dhaifu ya Diego Milito.

Mabingwa hao wa Europa League Atletico walikuwa katika hali nzuri kimchezo dhidi ya kikosi cha kocha wa zamani wa Liverpool Rafael Benitez katika mchezo huo.

Inter chini ya Bernitez walikuwa wakiwania taji la pili katika mchezo huo baada ya kufanikiwa kupata taji la Italian Super Cup juma lililopita kwa ushindi wa mabao 3-1dhidi ya Roma
.

Katika msimu uliopita Inter Milan chini ya Jose Mourinho walifanikiwa walifanikiwa kutwaa mataji matatu ya Champions League, Serie A na Italian Cup Treble.

RIO FERDINAND KUREJEA DIMBANI BAADA YA WIKI MBILIBaada ya kutamigwa kwa muda sasa,mlinzi wa kutumainiwa wa mashetani wekundu Rio Ferdinand anatarajiwa kurejea dimbani baada ya kuarifiwa kuwa hali yake inaendelea vizuri baada ya maumivu ya mguu.

Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31alipatwa na maswahibu ya maumivu akiwa mazoezini akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza June 4 maarufu kama “simba watatu” wakati wa maandilizi ya michezo ya kombe la dunia na kupelekea kuikosa michezo ya kombe hilo.
Hata hivyo kocha wa mashetani wekundu Sir Alex Ferguson anasema hakutegemea kumpata mlinzi wake huyo mpaka September.

Akikaririwa anasema "hatoweza kucheza katika mchezo wa jumamosi dhidi ya West Ham lakini tunatazamia kua naye katika kipindi cha kuanzia wiki mbili zijazo

Ferdinand aliumia baada ya kugongana na mchezaji mwenzake katika timu ya taifa Emile Heskey wakati wa mazoezi ya timu ya taifa kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia kule Rustenburg.

No comments:

Post a Comment