KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 3, 2012

Tottenham yamtangaza Andre Villa Boas kuwa meneja wao mpya

Andre Villa-Boas kocha mpya wa Tottenham Hospurs

Meneja wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas ameteuliwa kuwa meneja mpya wa Tottenham Hotspur ikiwa ni wiki tatu baada ya kuondolewa kibaruani kwa mtangulizi wake Harry Redknapp.
Villas-Boas mwenye umri wa miaka 34 anarejea katika medani ya soka akiwa na mkataba wa miaka mitatu katika kipindi kisicho zidi miezi minne tangu kuondoshwa Chelsea.
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc, Roberto Martinez wa Wigan, Fabio Capello na mshambuliaji wa zamani wa Spurs Jurgen Klinsmann walikuwa wakihusishwa na kazi hiyo.
Maisha ya Boas katika soka
    1977: Born in Porto 17 October
    1993: Works as a trainee under Sir Bobby Robson at Porto
    1994: Achieves Uefa C coaching licence in Scotland
    2002: Becomes part of Jose Mourinho's staff at Porto
    2004: Follows Mourinho to Chelsea
    2008: Moves with Mourinho to Inter Milan
    2009: Appointed manager of Academica
    2010: Named Porto boss
    2011: Wins league, cup and Europa League in first season
    2011: Appointed Chelsea manager
    2012: Sacked by Chelsea after a 257-day reign at Stamford Bridge
Tottenham imetoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa klabu hiyo wa Twitter.
Imenukuliwa taarifa hiyo kupitia mtandao huo ikisomeka "klabu ina furaha kumtangaza Andre Villas-Boas kama kocha mkuu,".
Maamuzi ya Tottenham kumfukuza kazi Redknapp yalikuwa ni baada ya wiki kadhaa za mvutano kati ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 na mwenyekiti wa klabu Daniel Levy.

No comments:

Post a Comment