KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 10, 2012

SIMBA YAELEKEA TANGA BILA YA NGASA, OKWI NA REDONDO.


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara Simba ya jijini Dar es Salaam imeondoka jijini hii leo na kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wao wa raundi ya saba dhidi ya Coast Union ya huko mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Mkwakwani Oktoba 13.

Simba wameelekea Tanga wakiwa ndio vinara wa ligi hiyo ya Tanzania Bara inayoshirikisha jumla ya timu 14 huku Simba wakiongoza baada ya kujikusanyia jumla ya alama 16 wakifuatiwa na Azam fc yenye alama 14.

Simba imeondoka bila ya wachezaji wake kadhaa muhimu akiwepo Mrisho Ngasa anayesumbuliwa na malaria kama ilivyo kwa Ramadhani Chombo Redondo ambaye naye anasumbuliwa na malaria.

Wengine walioachwa ni Haruna Shamte ambaye anasumbuliwa na enka, Kiggi Makassi mwenye matatizo ya goti pamoja na Abdalah Seseme na Waziri Hamadi.

Kwa upande wa mganda Emmanuel Okwi yeye anaelekea kwao Uganda kwa ajili ya majukumu ya kimataifa.
 
Waliondoka ni wachezaji 22 ambao ni,

MAKIPA:Juma Kaseja na Wilbert Mweta.

Walinzi: Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema, Koman Keita.

Viungo: Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban.

Washambuliaji:Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma.

RATIBA RAUNDI YA 7

10.10.2012. 43 LEO KAGERA SUGAR JKT RUVU KAITABA KAGERA
  11.10.2012. 44 TOTO AFRICANS YOUNG AFRICANS CCM KIRUMBA MWANZA
  13.10.2012. 45 POLISI MOROGORO AZAM JAMUHURI MOROGORO
  13.10.2012. 46 TANZANIA PRISONS JKT OLJORO SOKOINE MBEYA
  13.10.2012. 47 COASTAL UNION SIMBA MKWAKWANI TANGA
  13.10.2012. 48 RUVU SHOOTINGS AFRICAN LYON MABATINI PWANI
  13.10.2012. 49 MTIBWA SUGAR MGAMBO JKT MANUNGU MOROGORO
 

No comments:

Post a Comment