Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imesema kuwa imekubali matokeo ya mchezo wao wa jana wa ligi kuu Tanzania Bara ambapo mabingwa hao wa kombe la Kagame walilala kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam, kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Laurence Mwalusako amesema kuwa wamekubaliana na matokeo hayo ambapo amesema kimsingi mpira wa maguuu una matokeo ya aina tatu ambayo ni kufunga, kufungwa na kwenda sare.
Amesema kwasasa wanajipanga na mchezo ujao dhidi ya Toto utakao chezwa Alhamisi katika dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza.
Mwalusako amesema kuwa vipigo viwili vya ugenini vimewaumiza wao kama viongozi na kwasasa wanatafakari juu ya vipigo hivyo vya ugenini dhidi ya Kagera Sugar na Mtibwa na kwamba wanamuomba mungu waweze kushinda katika mchezo wao dhidi ya Toto Afrika na tayari baadhi ya viongozi wamesha fika katika jiji la Mwanza kuweka mambo safi kabla ya mchezo wao wa Alhamisi.
Hata hivyo Mwalusako amekanusha madai ya baadhi ya wadau kuwa pengine kitendo cha Yanga kubadili Kocha kimeathiri mwenendo wa matokeo ya timu yao kwa kuwa kocha msaidizi yuko na amekuwa akimpa mwongozo kocha wao mpya Brandts.
No comments:
Post a Comment