KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, November 15, 2012

KAMATI YA USHINDI YA SERENGETI YATEMBELEA MAZOEZI YA TIMU HIYO UWANJA WA TAIFA.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya Serengeti Kassim Dewji akiongea na wachezaji wa timu hiyo.
Kutoka ni wajumbe wa kamati hiyo Angetile Oseah, Selemani Nyambui, Henri Tandau na makamu mwenyekiti Kasim Dewji.
Kasim Dewji akisisitiza Jambo kwa wachezaji wa Serengeti huku kocha Jacob Michelsen na msaidi wake Jamhuri Kihwelu wakimsikiliza kwa makini.
Wachezaji wa Serengeti wakimfuatilia kwa karibu Kassim Dewji.
Kocha Jacob akiwa na Jamhuri Kihwelu wakifurahia neno kutoka kwa Kassim Dewji.



 
 Kamati maalumu iliyoundwa na Rais wa shirikisho la sika hapa nchini Leodigar Tenga hii leo imetembelea mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Hiyo ilikuwa ni sehemu ya kuihamasisha timu ya vijana ya Serengeti Boys ili iweze kufanya vizuri katika mchezo wake wa jumapili dhidi ya timu ya Vijana ya Congo Brazzaville ambayo tayari imeshawasili nchini toka jana kwa ajili ya mchezo huo.

Akiongea na wachezaji hao makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Kassim Dewji amewataka wachezaji hao kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya kocha Jacob Michelsen akisaidiana na Jamhuri Kihwelu ili kuwa na nidhamu nzuri ya kimchezo na hatimaye kupata matokeo mazuri katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini.

Dewji pia amewaambia wachezaji hao kuwa watanzania wanawategemea sana kuwapa ushindi katika mchezo huo na kwamba ana imani kubwa kuwa watajitokeza kwa wingi siku ya mchezo hivyo si vema wakaondoka uwanjani wakiinamisha vichwa chini.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama cha riadha hapa nchini Selemani Nyambui ambaye alipata nafasi ya kuongea na wachezaji hao amesema amefurahishwa sana na jinsi maandalizi ya mchezo huo yalivyo chukuliwa kwa uzito wa juu na hivyo ametaka wachezaji hao kuweka akili yote wanayofundishwa wa makocha wao.

Kambi ya timu ya taifa kuanzia hii leo imehamia katika hoteli ya JB Belmont kwa lengo la kuongeza hamasa ya kambi ambapo kesho wachezaji hao wameandaliwa chakula cha usiku katika mgahawa wa hoteli hiyo ambapo wachezaji hao watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na wadau mbalimbali wa soka.

Mwenyekiti wa soka la vijana kutoka TFF Alhaji Ahmed Msafiri Mgoy akiongea na Rockersports amesema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba kesho wanataraji kuwapoa waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Uganda na wamesha watafutia nafasi katika hoteli ya TANSOMA ambapo watafikia.

No comments:

Post a Comment