Lionel Messi akifuatana na mpenzi wake Antonella Roccuzzo muda mfupi kabla ya kujifungua. |
Hospitali aliyopelekwa Antonella Roccuzzo mpenzi wake Messi kwa maandalizi ya kujifungua |
Hapa wakila raha kabla ya ujauzito |
Messi ayapotezea mazoezi
ya Barcelona akimsubiri mtoto wake wa kiume Thiago mtarajiwa.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina
na klabu ya Barcelona Lionel Messi masaa machache yajayo anatarajia kutwa baba
kufuatia mpenzi wake ambaye ni mja mzito kukimbizwa hospitali kwa ajili ya
kujifungua.
Nyota huyo amepewa ruhusa na klabu
yake na kuachana na mazoezi ya leo kwenda kuungana na mpenzi wake Antonella
Roccuzzo kumsibiri kwa hamu mtoto wao wa kiume aliyepewa jina tayari la Thiago.
Roccuzzo amepelekwa katika hospitali
ya USP Dexeus mapema asubuhi ya leo na nyota Lionel Messi kujiunga naye katika
hospitali hiyo iliyokaribu na Camp Noun na hivyo kukosa mazoezi ya leo.
Kocha wa Barca Tito Vilanova amesema
bado haja amua kama Messi atakuwepo katika mchezo wa kesho wa ligi ya soka
nchini Hispania maarufu kama ‘Primera Division’ dhidi ya Celta Vigo kama mpenzi
wake atafanikiwa kujifungua muda mfupi ujao kabla ya mchezo.
Wenger sina nia ya
kulipiza kisasi cha mabao 8-2 kwa United.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kamwe hana nia ya
kulipiza kisasi kichapo alichokipata ambacho si rahisi kusahau toka kwa
mashetani wekundu katika mchezo utakao pigwa cha kuvumilika mwishoni mwa juma hili.
Washika mitutu hao walipata kichapo
takatifu cha mabao 8-2 toka kwa Manchester United msimu uliopita kichapo
ambacho kiliibua maswali mengi juu ya hatma ya Wenger na sasa anaingia katika
mchezo huo huku maswali yakiibuka juu ya uwezo wa safu yake ya ulinzi.
Safu ya ulinzi ya Arsenal iliruhusu
mabao manne ndani ya dakika 37 za mchezo wa kombe la ligi (siku hizi Capital
One) dhidi ya Reading mchezo uliofanyika jumanne huku pia rikodi ya meneja hiyo
baada ya michezo kumi na moja ikionekana kuwa ina mashaka.
Mwenyewe amenukuliwa akisema
"hiyo ni takwimu tu kuhusu mimi
lakini tunakwenda katika mchezo huo tukiwa tunajiani sana"
"siwezi kuzungumzia matokeo ya
mchezo wa msimu uliopita wakati tukielekea katika mchezo wa kesho ukizingatia
kuwa karibu asilimia tisini ya wachezaji watakao kuwepo kesho walikuwepo
walicheza katika mchezo wa msimu uliopita kule Old Trafford.
"ni kweli kuna hisia za
kimatokeo kama hivyo lakini suala la kulipiza kisasi si jambo ninalo lifikiria
katika mchezo huo. Kisoka hilo la matokeo ya aina hiyo si muhimu sana.
"suala la ulinzi wakati wa
mchezo si jibu la udhaifu wa kikosi , lakini pia uwezo wa mpinzani pia. Unatakiwa
kupongeza kama una ubora katika sehemu ya ulinzi katika katika ligi na
ninachoweza kuahidi ni kwamba tumeifanyia kazi safu yatu ya ulinzi.
Wenger anaamini kikosi chake kinaweza
kuyaleta matokeo ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wapinzani wao wa kutoka London
ya kaskazini Tottenham katika mchezo wa ligi uliopita mpaka Old Trafford watakapo
kuwa wakikabiliana kwa mara ya kwanza na mshambuliaji wake wa zamani uso kwa
uso Robin van Persie tangu ajiunge na United msimu huu akitokea Arsenal.
Esperance kumkosa Msakni
anasumbuliwa na mguu
Esperance itakuwa dimbani bila ya
nyota Youssef Msakni katika mchezo wa kwanza wa fainali ya ligi ya mabingwa barani
Afrika dhidi ya Al Ahly mchezo utakao pigwa hapo kesho.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wsa
miaka 21 alifanyiwa upasuaji hapo jana baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa ‘appendicitis’
na hivyo hatakuwepo katika kikosi kitakacho elekea nchini Misri.
Kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa
watunisia hao ambao wamedhamiria kutetea taji hilo walilolitwaa msimu uliopita.
Msakni ameifungia Esperence jumla ya
mabao manne katika michuano hiyo msimu huu.
Aidha Esperance tayari imeshakubali kumuuza mshambuliaji
huyo baada ya mchezo wa fainali ambapo inaarifiwa kuwa mchezaji huyo ameridhia
kujiunga na Lekhwiya ya nchini Qata mwezi January mwakani.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tunisia
ni miongoni mwa wachezaji ambao wametajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora barani
Afrika.
Al Hilal kumaliza nuksi
ya kuishia nusu fainali kombe la shirikisho
Al Hilal ya Sudani inatarajiwa
kumaliza balaa la kuishia katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho
barani Afrika ambapo hii leo watakuwa wenyeji wa Djoliba ya Mali katika mchezo
wa kwanza wa nusu fainali.
Ndani ya kipindi cha miaka mitano Hilal
imepoteza mara tatu katika ligi ya mabingwa Afrika na kuishia katika hatua ya
nusu fainali na mara moja katika kombe la shirikisho.
Klabu hiyo ya nchini Sudani ilimaliza
katika nafasi ya pili katika kundi A na ikijikuta ikicheza na mshindi wa kundi
la B Djoliba ya Mali.
AC Leopards itakuwa mwenyeji wa Al
Merreikh katika mchezo wa nusu fainali nyingine utakapigwa jumapili.
Baada ya kuhaha katika miaka ya hivi
karibuni , Hilal itataka kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kupata matokeo ya
kushiba kabla ya mchezo wa pili wa marudiano utakao pigwa wiki mbili zijazo
nchini Mali.
Hilal, ambayo imesheheni nyota kibao
kutoka mataifa ya Cameroon, Equatorial Guinea, Mali, Nigeria, Senegal na Zimbabwe,
iliwachapa wa-Mali wengine kule Bamako katika mchezo wa ‘play-off’ na kutinga
hatua ya makundi.
Wakiongozwa na kocha raia wa nchi
mbili Ufaransa na Italia Diego Garzitto, Hilal ilisonga mbele katika hatua ya
makundi mpaka hatua ya nusu fainali baada ya kupata matokeo ya ushindi michezo
minne, sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.
Mshambuliaji raia wa Zimbabwe Edward
Sadomba amekuwa chachu ya ushindi ya timu hiyo akifunga mabao matano mwaka
mmoja baada ya kumaliza akiwa mfungaji bora kwa kufunga magoli saba katika ligi
ya mabingwa msimu uliopita.
Djoliba imeingia hatua hiyo baada ya
ushindi wake wa nyumbani na ugenini dhidi ya mshindi wa pili bingwa wa michuano
ya vilabu bingwa mwaka jana 2011 Wydad Casablanca.
No comments:
Post a Comment