KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 2, 2012

STEWART JOHN HALL: NIMEKIMBIA NJAA SOFAPAKA LAKINI PIA WACHEZAJI WA AZAM WALINIPIGANIA NIREJESHWE.

Kocha mkuu wa Azam fc Stewart John hall aliyerejea katika klabu hiyo juzi akitokea Sofapaka ya nchini Kenya amesema tangu ajiunge na klabu ya Sofapaka alijikuta akiishi maisha ya shida kwa kuwa klabu hiyo ilishindwa kumlipa  mshahara wake.

Stewart amesema mbaya zaidi klabu hiyo ilikuwa hailipi mishahara hata ya wachezaji wake jambo ambalo lilianza kumuingiza katika hali ngumu katika kazi yake ya ufundishaji ndani ya klabu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa timu yake ya Azam dhidi ya Coast Union ya Tanga mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam Complex na Azam kuvuna karamu ya mabao 4-1, Stewart amesema kimsingi maisha yalikuwa ni tofauti na alivyokuwa katika klabu ya Azam ambayo imeamua kumrejesha katika kazi hiyo baada ya kumtimua aliyekuwa mrithi wake Boris Bonjak.

Kocha huyo ametanabaisha kuwa anaipenda sana Azam na kwamba  hata alipo ambiwa kuwa kibarua chake kilikuwa kimeota nyasi baada ya kutokea kutokuelewana baina yake na viongozi eti kwasababu ya namna ya kupanga kikosi ilimsikitisha sana kwa kuwa aliondoka wakati wachezaji walikuwa wakimpenda sana.

Katika kuthibitisha hilo jana mara baada ya bao la nne lililofungwa na Hamisi Macha Viali, wachezaji wa timu hiyo walimkimbilia kocha huyo huku wakipiga makofi na kuimba jambo ambalo Stewart aligusia kuwa ni zilikuwa ni salamu za wachezaji hao kuwa na mapenzi makubwa na yeye.

Amesema wakati akiwa nchini Kenya alikuwa akiwasiliana na baadhi ya wachezaji wake hao ambao wengi walikuwa wakionyesha waziwazi kumtaka arejee, jambo ambalo wachezaji hao waliendelea kushinikiza uongozi kumrejesha na ndipo klabu ya Azam ilipo amua kumtimua Boris Bonjak na kumrejesha Stewate John Hall.

Amesema mpango wake ni kuhakikisha Azam inakuwa bingwa wa taji la kuu msimu na kwamba jambo hilo linawezekana kwani  nafasi iliyopo katika msimamo wa ligi ni nzuri licha ya ushindani kuwa mkubwa na timu nyingi kucheza vizuri tofauti na misimu miwili ya huko nyuma.

Amesema amefurahia viongozi wake wamesahau yaliyopita na sasa wameonyesha wazi kutaka kumpa ushirikiano katika kazi yake na yeye kwa moyo wake wote yuko tayari kutumia utaalamu wake katika kufanikisha azma yake ya kutwaa taji.

No comments:

Post a Comment