Neymar: kucheza
timu moja na Messi itakuwa ndoto.
Mshambuliaji
wa Santos ya nchini Brazil Neymar, ameweka wazi kuwa itakuwa ndoto yeye kucheza
akiwa pamoja na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi.
Mbrazil huyo
kwa kipindi kirefu alikuwa akihusishwa kutaka kuelekea Camp Nou, na hivi karibuni Peixe alikaririwa akisema mpango wa uhamisho ulikuwa tayari kwa kijana huyo kuelekea kwa kigogo hicho cha Catalunya.
Hata hivyo
mshambuliaji huyo mbichi na mwenye uwezo mkubwa akiwa na umri wa miaka 20 kwa
mara nyingine ameondosha matumaini hayo na kwamba kikosi cha Tito Vilanova
kinaweza kuwepo katika fikra zake endapo ataamua kuachana na soka la Marekani
ya kusini.
Amenukuliwa na
gazeti la Marca akisema,
"kucheza
na Messi itakuwa ndoto. Labda kufanya na ye mazoezi hiyo nitafurahia sana,".
Mshambuliaji
huyo kijana anaamini kwamba wakati Cristiano Ronaldo na Andres Iniesta wakiwa
katika kiwango cha juu na wachezaji wakubwa duniani kwasasa lakini anaamini
kuwa hakuna anayestahili tuzo ya Ballon d'Or zaidi ya Messi.
"kwa
upande wangu kuna wachezaji watatu ambao ni wazuri sana kuliko wengine, Iniesta,
Ronaldo and Messi," "lakini Messi ndiye bora. Hakuna mtu anayeweza
kufanya vitu anavyo fanya."
Neymar pia
amemshukuru Messi ambaye mtaja yeye kuwa ndiye atakaye fuatia kuchukua tuzo
hiyo kwa kusema ni mchezaji mzuri "excellent footballer".
"unadhani
mchezaji kukusifia? Imenifurahisha namshukuru kwa maneno yake".
Ronaldinho anusurika katika ajali.
Nyota wa Atletico
Mineiro Ronaldinho amenusurika katika ajali ambayo ilihusisha magari matatu.
Wakati ajali
hiyo ikitokea kiungo huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akiendesha gari
kuelekea katika uwanja wa mazoezi ya timu yake.
Mbrazil huyo alinusurika kufa katika ajali hiyo kufuatia gari
lake kukwepa wakati ambapo mmoja kati ya medereva wa ajali hiyo
alikimbizwa katika chumba cha unagalizi wa dharura baada ya kugongana.
Gari ambalo
lilihusika moja kwa moja na ajali hiyo liliharibika vibaya lakini abiria
wamenusurika.
Mchezaji mwenzake
Jo aliyepita katika eneo la ajali hiyo la Lagoa Santa, alithibitisha kuwa Ronaldinho
alipona na kwamba alifika katika uwanja wa mazoezi ndani ya muda muafaka.
Mchezaji huyo
bora wa dunia wa zamani ambaye yuko katika kiwango cha juu katika klabu ya Atletico
akiwa amekwisha kufunga magoli saba msimu huu, anatarajiwa kuwepo dimbani jumapili
katika mchezo wa ugenini dhidi ya Coritiba.
Mouronho: sijui nitakuwa wapi baada
ya Real Madrid.
Kocha wa Real
Madrid Jose Mourinho amesema kuwa bado hajajua muelekeo wake baada ya kuondoka
katika klabu hiyo.
Baada ya
kushinda taji la ligi kuu ya nchini Hispania akiwa Los Blancos, mreno huyo
amekuwa kocha wa kwanza katika historia kushinda mataji makubwa ya ligi za ndani
katika nchi za Italia, England na Hispania.
Mourinho ameweka
wazi njaa yake ya kutaka kuendeleza mafanikio katika soka.
Amenukuliwa na
jarida la Ronda Ibera akisema,
"tangu
nikiwa mdogo nilijua kuwa ili kuendelea katika kazi yangu ni lazima nitembee
katika mataifa mengine. Nilijua nahitaji kusafiri, kukutana na changamoto mpya
ili niweze kukuwa"
"nilipo
anza kusafiri , dhamiri yangu ilikuwa katika mataifa ya England, Italia na Hispania. Nitakapo
ondoka hapa Real Madrid, sijui nitaelekea nielekee wapi katika kazi yangu.
"bado
najipigania, siku zote nataka kufanya vizuri. Hivyo basi nafikiria wengine na
hilo linanisaidia.
"ugumu
wa kufundisha unaongezeka siku hizi. Kocha wa leo hawezi kuwa katika uwezo ule
ule kama ilivyo miaka 10, 20 au 30 iliyopita.
"ugumu
wa kocha unakuwa katika kuchagua wachezaji 11, kufundisha mbinu na kufanya
mabadiliko."
Mourinho pia
akazungumzia jinsi ambavyo soka linavyo athiri maisha yake ya kawaida
akuzungumzia juu ya namna anavyo jitoa katika kufikia mafanikio.
"mtoto
wangu hawezi kwenda chuo bila wengine kumjua yeye ni nani. Mke wangu anataka nibakie
ndani ya gari wakati akiingia madukani kufanya ‘shopping’.
"hii
inanigharimu katika kufanikisha uweledi katika kazi yangu ninayo ipenda. Nimekuwa
nikihusika na soka tangu nimezaliwa. Sasa nakaribia miaka 50 umri ambao una
maana kubwa.
No comments:
Post a Comment