KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, July 1, 2013

Mlinda mlango mkongwe Mark Schwarzer aihama Fulham

Schwarzer mwenye umri wa miaka 40, ambaye alijunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru mwaka 2008 akitokea Middlesbrough, ni mlinda mlango wa kwanza kutoka nje ya England kudaka michezo 500.

Mlinda mlango mkongwe wa Fulham Mark Schwarzer amatarajia kuihama klabu yake ya Fulham baada ya kukataa kuongezewa mkataba mpya na klabu hiyo.
 
Fulham ilimsainisha mlinda mlango raia wa Uholanzi Maarten Stekelenburg kutoka klabu ya AS Roma kwa ada ambayo haikuwekwa wazi mwezi uliopita.

Schwarzer mlinda mlango wa kimataifa wa Australia amekuwa akidakia kikosi cha kwanza.

Schwarzer si mchezaji wa kwanza wa kikosi cha kwanza kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Wengine waliondoka ni pamoja na mlinzi wa kimataifa wa Ireland ya kaskazini Chris Baird, kiungo wa kimataifa wa Ugiriki Giorgos Karagounis, mshambuliaji wa Croatia Mladen Petric na nyota wa kimataifa wa Wales Simon Davies.

Fulham imewasajili tayari mlinzi wa Venezuela Fernando Amorebieta akitokea klabu ya Athletic Bilbao na kiungo wa Derek Boateng Dnipro ya Ukraine kwa uhamisho huru.

No comments:

Post a Comment