Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa
beki wa kimataifa wa Ivory Cost Kolo Toure kutoka Manchester City.
Toure mwenye miaka 32 amesajiliwa na
Liverpool kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba na Man City
wanaomilikiwa na kampuni ya Etihad kumalizika.
Ameichezea City jumla ya michezo 102
baada ya kusajiliwa akitokea Arsenal mwaka 2009 kwa pound milioni 14, lakini
alicheza mechi 18 pekee msimu uliopita na kujikuta akiachwa kwenye kikosi cha
wachezaji wa Man City walioshiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kolo Toure anaenda Merseyside baada
ya aliyekuwa nahodha msaidizi wa klabu hiyo Jamie Carragher kutundika daruga
huku hatma ya beki kitasa wa timu hiyo rais wa Slovakia Martin Skrtel ikiwa
haijulikani.
Ameuambia mtandao wa klabu hiyo hatua
hiyo ina maana kubwa kwake, na amejiunga na moja klabu bora nchini England.
"Nilipoondoka City ilikuwa ni
muhimu kwangu kubaki England kwa kuwa ni ligi bora na kuja Liverpool ni hatua
kubwa kwangu."
"Nimeichagua Liverpool kutokana
na historia yake na hamasa ya wachezaji wanavyoitumikia timu yao." Alisema
Toure.
Katika misimu saba aliyocheza
Arsenal, Toure alishinda Kombe la FA mara mbili na alikuwa miongoni mwa kikosi
cha Arsenal ambacho kiliandika historia ya kucheza ligi ya 2003-04 bila
kufungwa hata mechi moja.
Mwaka 2011 alikosa kombe la FA
walilochukua Man City kwa kufungiwa miezi sita kutokana kushindwa kufanya
vipimo vya madawa ya kuongeza nguvu michezoni.
Toure ni mchezaji wa nne kusajiliwa
na Liverpool baada ya klabu hiyo kumsajili, Luis Alberto na Lago Aspas pamoja
na mlinda mlango Simon Mignolet aliyesajiliwa akitokea Sunderland.
Swansea City yakamilisha usajili wa Jonjo Shelvey kwa pauni milioni £5 .
Swansea City imekamilisha usajili wa
kiungo Jonjo Shelvey kutoka klabu ya Liverpool kwa uhamisho wa pauni milioni £5.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21
ambaye aliichezea England kwa mara ya kwanza dhidi ya San Marino oktoba 2012, amesaini
mkataba wa miaka minne.
Crystal Palace iliyokuwa pia katika
vita ya kumnasa kiungo huyo sasa wamesalimu amri.
Shelvey ambeye ameichezea Liverpool
kwa michezo 17tangu ajiunge nayo akitokea Charlton Athletic mwaka
2010, anakuwa mchezaji wa sita wa kudumu wa Swansea kusajiliwa msimu huu wa
kiangazi.
Ametuma salamu kwa mashabiki wa Liverpool
kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akisema "Nitalikumbuka sana jiji na klabu pia asanteni sana, ni wakati wa kufungua ukurasa mpya wa
maisha yangu kule Wales. Asanteni."
BAADA YA KUJIUNGA NA REAL MADRID ISCO ANA MATUMAINI YA KUPATA NAFASI
YA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA
Isco wa Real Madrid anamatumaini kuwa
kuhama kwake kutamuongezea nafasi ya kucheza katika kombe la dunia akiwa na
kikosi cha timu ya Hispania
Amejiunga na klabu hiyo akitokea Malaga
kwa ada ailiyoripotiwa ya pauni £23 na kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na
meneja mpya Carlo Ancelotti.
Isco amesaini mkataba wa miaka mitano
baada ya kufanikiwa katika vipimo vyake afya.
Born: Benalmadena, Spain, on 21 April 1992
Clubs: Valencia B, Valencia, Malaga, Real Madrid
International: Spain - one appearance
Isco amekabidhiwa jezi nambari 23 namba
ambayo ilikuwa ikitumiwa na David Beckham wakati akiitumikia Bernabeu.
Amenukuliwa akisema
"Sote tunamjua Beckham ni
mchezaji mkubwa na aliitumia kwa miaka 10, lakini nimechagua namba hii kwasababu
ni siku ya kuzaliwa kaka yangu ".
Vito Mannone asajiliwa na Sunderland akitokea
Arsenal
Sunderland imemsajili mlinda mlango
wa Arsenal Vito Mannone kwa ada ambayo haikuwekwa wazi.
Mannone mwenye umri wa miaka 25, alijunga
na Atalanta mwaka 2005, na kuvichezea vilabu vya Barnsley na Hull City kwa
mkopo.
Mchezo wake wa mwisho uliokamilisha
utumishi wake wa michezo 26 ulikuwa ni baina ya Arsenal na Fulaham mchezo
uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 mwezi November 2012.
Kuwasili kwake kwa mkataba wa miaka
miwili kunafuatia kuondoka hivi karibuni kwa mlinda mlango nambari moja Simon
Mignolet kuelekea Liverpool kwa pauni milioni £9.
Mannone aliaanza kuichezea Arsenal miaka
minne baada ya kujiunga nayo akitokea Barnsley katika msimu wa mwaka 2006-07.
Nigeria yatolewa kombe la dunia.
Matumaini ya Nigeria yan kuchukua kwa
mara ya kwanza taji la kombe la dunia kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20
yamemalizwa na Uruguay katika hatua ya mtoano ya timu 16 za mwisho katika
michuano ambayo ambayo inafanyika nchini Uturuki.
Nigeria maarufu kama Flying Eagles ilipunguzwa
wachezaji wake na kusaliwa na wachezaji 10 uwanjani kabla ya mapunziko
imepoteza mchezo huo kwa kuachapwa mabao 2-1.
Nicolas Lopez alifunga magoli yote
mawili ya Uruguay likiwemo moja la penati ilhali Olarenwaju Kayode alifanikiwa
kufunga goli kwa upande wa Nigeria.
Ghana inakuwa ndiyo timu ya mwisho
kutoka katika bara la Afrika kusalia katika michuano hiyo na hii leo wanakabiliwa na
mchezo wa hatua hatua hiyo dhidi ya Ureno.
Mali na mabingwa wa African Misri
zimeshindwa kuvuka na kuingia katika hatua hiyo inayofanyika nchini Uturuki.
No comments:
Post a Comment