KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 19, 2014

Anderson anasema siku zote atakuwa ni sehemu ya United

 Kiungo Anderson Luis de Abreu Oliviera ameweka wazi sababu zake za kujiunga na Fiorentina kwa mkopo lakini ameshukuru wote waliomuunganisha na Manchester United na kumpa sapoti katika kipindi chote cha miaka sita na nusu ndani ya klabu hiyo.
Kiungo huyo ameitumikia United kwa michezo minne tu tangu meneja wa sasa kurithi mikoba ya mtangulizi wake Sir Alex Furguson.
Anderson alicheza mchezo mmoja tu ambao alikamilisha dakika zote 90 tangu kuanza kazi kwa David Moyes akishindwa kufurukuta kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Anderson amesema kuelekea kwake Italia ambako kunajumuisha makubaliano ya mauzo mwishoni mwa msimu ilikuwa ni lazima kufanyika hivyo kwani alikuwa akisaka nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza huku akitanabaisha kuwa siku zote atakuwa ni sehemu ya familia ya United.

"Asante United kwa yote uliyonipatia, ilikuwa furaha na nikijivunia kuwa sehemu ya klabu kubwa" Ameandika hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

"Sitasau wenzangu na marafiki zangu, wote ni watu muhimu wazuri ambao tulifanya nao kazi kwa pamoja, Love you all and you always be in my heart.

"Wish you all the best because we always be together United family! Now I have to leave because I really need to play.

"Asante pia Fiorentina kwa kunipa fursa hii na kuniamini. hamtajutia kwasababu nitawata yote kwa asilimia 100% "

No comments:

Post a Comment