KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, January 19, 2014

Real Madrid wakamilisha idadi sawa na vinara wa La Liga Barca na Atletico Madrid muda mfupi kabla hawajashuka dimbani nini kitatokea baadaye

Gareth Bale amefanikiwa kufung kwa mara ya kwanza kwa taribani kipindi cha miezi miwili kupita katika mchezo ambao Real Madrid imefanikiwa kufikisha idadi sawa ya alama na waliokuwa viongozi wa masimamo hapo kabla Barcelona na Atletico Madrid katika ligi kuu ya Hispania Liga. 
Mshindi wa tunzo ya Ballon d'Or Cristiano Ronaldo amekuwa katika wiki nzuri ambapo hii leo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzamisha mpira wavuni dhidi ya kikosi kinacho kamata mkia wa ligi hiyo Real Betis.
Bale, ambaye kwa mara ya mwisho kufunga ilikuwa ni katika mchezo dhidi ya Valladolid Novemba 3-0, ndiye alitengeneza bao la kwanza kwa mpira mzuri wa moja kwa moja (superb free-kick) kabla ya Karim Benzema kuandika bao lake la 100 akiifungia Madrid.

Ancelotti amekiongoza kikosi cha Real Madrid mpaka kufikia mchezo wa 18 bila kufungwa katika michuano yote tangu mara ya mwisho kufungwa kwa bao 2-1 na Barcelona Oktoba 26.

Carlo Ancelotti alijua kuwa ushindi kwake utakuwa unaongeza presha katika usukani wa ligi ambapo waliokuwa vinara kwa muda mrefu Barca na Atletico, usiku huu watakuwa dimbani kupambana dhidi ya Levante na Sevilla.

Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo, ambaye alifunga goli Jumatano dhidi ya Osasuna katika mchezo wa Copa del Rey alishangilia bao lake la 21 la msimu huu akipoga mpira wa mbali. 

No comments:

Post a Comment