Fernando Llorente afurahia kiwango cha timu yake lakini awaonya wachezaji wenzake
Mshambuliaji wa Juventus Fernando Llorente amekitaka kikosi chao kuendeleza wimbi la ushindi baada ya ushindi mwanana wa mabao 4-2 dhidi ya Sampodoria.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Athletic Bilbao ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi kwa timu yake likiwa no goli lake la nane huku mengine yakifungwa na Paul Pogba na Arturo Vidal aliyefunga mabao mawili na kuufanya kuwa ni ushindi wa 12 mfululizo kwa mabingwa hao watetezi wa taji la ligi hiyo ya Italia 'Serie A'.
Llorente ameweka wazi kuwa anavutiwa mno na kiwango cha klabu yake maarufu kama Biancocelesti lakini akaonya kuwa wanatakiwa kuendeleza ushindi na katu wasiruhusu kiwango chao kushuka hususani kati huu wakijiandaa kwa mchezo wa robo fainali ya Coppa Italia dhidi ya Roma.
No comments:
Post a Comment