Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema
shirikisho lake limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu
ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
Malinzi
ameeleza mikakati hiyo ya uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu)
wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake
jijini Dar es Salaam.
Amesema
uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu
ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa
(Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.
Kwa
upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini
yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya
Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira
wa miguu duniani.
CAPTION:
Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa
zamani Edward Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake
katika kuinua kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo
umefanyika leo (Januari 20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment