Young
Africans imekamlisha ziara ya kambi yake nchini Uturuki bila ya
kupoteza mchezo hata mmoja baada ya leo kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi
ya timu ya Simurq PIK inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbajain katika
mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jioni ya leo katika viwanja
vya Side Star Hotel Complex Manavgat jijini Antalya Uturuki.
Mchezo
wa leo dhidi ya Simurq PIK ulikuwa ni mchezo wa nne kwa Young Africans
tangu kuwasili nchini Uturuki ambapo imeweza kushinda michezo mwili
dhidi ya Ankara Sekerspor 3-0, na Altay SK 2-0 zote za Ligi Daraja la
pili nchini Uturuki kabla ya kutoka sare na timu ya KS Flamurtari ya
Ligi Kuu nchini Albania.
Dakika
ya 13 ya mchezo mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi, Didier
Kavumbagu aliipatia Young Africans bao la kwanza kufuatia pasi nzuri ya
mshambulaji Emmanuel Okwi na Didier kuukwamisha mpira wavuni na
kumuacha mlinda mlango wa Simurq PIK Pawel Kapsa akiduwaa.
Simuriq
PIK walifanya shambulizi kupitia kwa kwa kiungo wao Stephan Polyak
lakini golikipa wa Young Africans Juma Kaseja alikoa hatari hiyo, huku
Tagim Novruzov akishindwa kumalizia mpira uliotoka sentimeta chache
langoni.
Dakika
ya 30 ya mchezo Young Africans ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa
kiungo Mrisho Ngasa ambaye aliwatoka walinzi wa Simurq kufuatia migongeo
mizuri katika Niyonzima, Okwi , Kavumbagu na kumkuta Ngasa ambaye
aliukwamsiha mpira katika nyavu ndogo.
Mpira
wa krosi uliopigwa na nahodha wa Simurq Ruslan Poladov uliwapita
walinzi wa Young Africans wakishindwa kuucheza na kumkuta mlinzi wa kati
Anderson Oliveira aliyepanda kusaidia mashambulizi aliyeipatia timu
yake bao la kusawazisha.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwaza, Young Africans 2 - 1 Simurq PIK.
Kipindi
cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Nadir
Haroub "Cannavaro" aliingia kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani huku
kiungo Hamis Thabit akichukua nafasi ya kiungo mkabaji Frank Domayo
"Chumvi".
Dakika
ya 56 ya mchezo Simuriq PIK walipata bao la pili na la kusawazisha
kupitia kwa mshambulaji wao Murad Sattarli baada ya kazi nzuri
iiyofanywa na kiungo wao Stephan Polyak na mpira huo kuwapita walinzi wa
Young Africans na kumkuta mfungaji.
Mara
baada ya bao hilo, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini
mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 2 Simurq PIK.
Mara
baada ya mchezo wa leo kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van
Der Plyum amesema vijana wake wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo,
ana muda wa wiki moja lakini tayari anaona mabadiliko kiuchezaji na
kutegemea kufanya vizuri katika mashidano yatakayotukabili.
"Timu
imecheza vizuri nawapongeza vijana kwa kujituma, hakuna lisilowezekana
katika mpira, wachezaji wangu sasa hivi wanajiamini na wanajua
wanatakiwa wafanye nini kwa wakati muafaka, ilikua mechi nzuri sana hata
kocha wa Simurq PIK amefurahi uwezo wetu" alisema Hans.
Mara
baada ya mechi ya leo timu itaendelea na mazoezi kesho asubuhi
kuendelea kujiweka fit kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini katikati
ya wiki hii tayari kwa ajili ya mzunguko wa Pili wa Ligi Kuu ya Vodacom
na mashindano ya kimataifa.
Young Africans:
1.Juma Kaseja, 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Mbuyu Twite, 5.Kelvin
Yondani/Nadir Haroub, 6.Frank Domayo/Hamis Thabit, 7.Mrisho Ngasa/Saimon
Msuva, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier Kavumbagu, 10.Emmanuel Okwi,
11.David Luhende/Said Bahanuzi
Simurq PIK:
1.Pawel Kapasa, 2. Ruslan Poladov , 3.Dilaver Zrnanovich, 4.Tural
Axundov, 5.Anderson De Oliveira, 6.Tagim Novruzov, 7.Nichat
Kurbanov/Bashir Jamilu, 8.Patrick Osiako, 9.Salif Ballo, 10.Rashad
Ayyubov, 11.Stepahn Polyak
No comments:
Post a Comment