Mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia hatua ya 16 bora wa Mashindano ya Klabu
Bingwa Barani Afrika kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya National Al Ahly utafanyika kesho katika Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam huku tayari tiketi za mchezo huo zikinunuliwa kwa wingi na
wapenzi wa soka kwa ujumla.
Young Africans ambao ndio wawakilishi pekee wa mashindano ya
kimataifa nchini Tanzania kawa sasa watashuka dimbani kesho kwa lengo
moja tu la kuhakikisha historia inaandikwa kwa kuvunja mwiko dhidi ya
Waarabu na kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kikosi cha
Mholanzi Hans Van de Pluijm kimekuwa kikiendelea na mazoezi asubuhi na
jioni katika Uwanja wa Boko Beach kujiandaa na mchezo huku morali ya
wachezaji ikiwa ni ya hali ya juu, saikolojia na kimwili wakiwa tayari
kwa mechi.
Kuelekea mchezo wa kesho mchezaji pekee ambaye
atakosekana ni Rajabu Zahir kutokana na kupata maumivu ya kuchanika
nyama za msuli wa paja
National Al Ahly ambao waliwasili jumatano
asubuhi, hii leo wameendelea na mazoezi yao katika
Uwanja wa Taifa kama sheria za shirikisho la soka duniani FIFA zinavyosema tayari kwa kuuzoea kwa mchezo huo wa kesho baada ya hapo awali baada ya kuwasili kuanza kufanya
mazoezi kwa siku mbili katika shule ya IST Upanga.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao rasmi ya klabu ya Yanga ni kwamba uongozi wa
Young Africans umejiandaa na kuhakikisha kila kitu kinakwenda salama kwa
upande wa wachezaji, utawala na washabiki watakaojitokeza kushuhudia
mchezo huo ulioteka hisia za wapenzi wengi wa soka barani Afrika.
Katika hatua nyingine Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri yake kwenye mechi
yake ya kwanza ya raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly
kutoka Misri.
Mechi
hiyo inachezwa kesho (Machi 1 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia
10 kamili jioni. Timu hizo zitarudiana Machi 9 mwaka huu jijini Cairo, Misri.
Maandalizi
ya mechi hiyo yamekamilika ambapo kamishna Abbas Sendyowa kutoka Uganda na
waamuzi wanne kutoka Burundi tayari wapo nchini kwa ajili ya mechi hiyo
inayotarajiwa kuvuta maelfu ya washabiki.
Milango
yote katika uwanja huo itakuwa wazi, ukiwemo ule wa upande wa Uwanja wa Ndani
(Indoor Stadium) wakati Barabara ya Taifa (Taifa Road) itafungwa kuanzia chuo
cha DUCE hadi msikitini kuanzia saa 4 asubuhi.
Magari
maalumu yenye sticker pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani. Vilevile
washabiki wanakumbushwa kuwa hawaruhusiwi kuingia uwanjani wakiwa na silaha au
vifaa vyovyote vya chuma.
Watanzani wote bila kujali itikadi zao za vilabu kwa ujumla wameombwa kujitokeza kwa
wingi kesho kwa lengo la kuiunga mkono Ynaga kwani ndio timu
pekee inayowakilisha nchi na kupeperusha bendera ya Taifa katika
mashindano ya kimataifa ya vilabu barani Afrika.
No comments:
Post a Comment