KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 22, 2014

GEOFREY NYANGE KABURU AMSAINISHA KOCHA LOGARUSIC MKATABA WA MWAKA MMOJA SIMBA

Makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu
Uongozi wa klabu Simba umemuongezea mwaka mmoja kocha mkuu wa klabu hiyo Zdravko Logarusic baada ya kuhitimisha mkataba wa awali nusu mwaka.
Akiongea hii leo katika makao makuu ya klabu hiyo, makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu amesema uongozi wa Simba umeridhishwa na kocha Logarusic na kwamba kuanzia sasa atakuwa akisimamia timu zote ya wakubwa na vijana akisaidiana na kiungo za zamani wa klabu hiyo Selemani Matola.
Kaburu amesema ndani ya mkataba mpya na Loga kunaweza kukafanyika mabadiliko ya ama kumfuta kazi au kumuongezea muda zaidi kutegemeana na makubaliano ya kimsingi ambayo ni pamoja na uwezo wa kiuchezaji wa kikosi cha Simba.
Kocha Loga wa Simba.
Kaburu amesema wanaamini kuwa kocha huyo atairejesha klabu yao katika heshima yake kama ilivyokuwa huko nyuma, ambapo Simba kama itakumbukwa ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Kwa upande wake kocha Loga ameahidi kufanya mazuri kubadilisha soka na matokeo ya Simba kwani ni klabu kubwa ambayo ina mashabiki wengi ambao wana presha kubwa nyuma yake.