LIGI DARAJA LA KWANZA NETBALL: TIMU YA JKT MBWENI YATAWAZWA KUWA MABINGWA 2014/15
  | 
| JKT Mbweni wametawazwa kuwa mabingwa wa michuano ya ligi daraja la kwanza 2014/2015 kufuatia ushindi wa magoli 32-23 dhidi ya timu ya Uhamiaji katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Mbali na kikombe cha Ubingwa pia washindi wapya JKT Mbweni wamezadiwa 
shilingi laki nne kutoka kwa wadhamini kampuni ya vinywaji baridi ya 
Pepsi ambao pia walitoa fulana kwa washindi wa kwanza mpaka watatu. Anna
 Kibira mwenyekiti wa chama cha mchezo wa netball nchini Tanzania 
CHANETA amesema mashindano yalikuwa mazuri na kusisimua, ambapo 
amevishukurua vilabu vyote ambavyo vimeshiriki mashindano hayo ambao 
wamepokea vyeti vya ushiriki wao. | 
 
 
 
          
      
 
  
No comments:
Post a Comment