Arsene Wenger akimsukuma Jose Mourinho kifuani kunako dakika ya 20 katika mchezo uliopigwa darajani Stamford Bridge Jumapili ya leo |
Upinzani baina ya Arsene
Wenger na Jose Mourinho umechukua sura mpya katika dimba la Stamford Bridge Jumapili ya leo baada ta meneja wa Arsenal kumsukuma mwenzake licha ya kuamuliwa na hali ya mambo kurejeshwa katika usalama bado wawili hao walishindwa kupeana mikono baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo.
tukio hilo lilitokea kufuatia Wenger
kukasirishwa na kitendo cha Gary Cahill kumkabili visivyo mshambuliaji wake Alexis Sanchez kunako dakika ya 20 ambapo mlinzi huyo wa Chelsea alizawadiwa kadi ya njano na mwamuzi kwa kile kilichoonekana alikuwa amefanya madhambi makubwa.
Meneja mfaransa Wenger kwa hamaki kubwa aliondoka katika eneo lake la ufundi la kumdhihaki mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkinson na kisha kumuonyesha mkono wa dharau meneja wa Chelsea Mourinho aliyekuwa anaelekea upande wake.
Wenger akibwatukiana na meneja wa Chelsea Mourinho darajani
Wawili hao walitenganishwa na mwamuzi wa akiba Jonathan Moss wakati makabiliano yalipojitokeza tena hii leo Daraji Stamford Bridge( tumia neno 'dugout')
Wenger mwenye umri wa miaka 64, alimsukuma Mourinho kifuani huku meneja wa Chelsea Mourinho ambaye ni mdogo wa kwa miaka 13
nyuma ya Wenger.
Meneja huyo wa Arsenal baadaye aligeuka na kutaka kuondoka kabla ya kurejea tena akiwa ameweka mikono mfukoni na kuanza kubwatukiana kama mnyama mbwa kimya kimya dhidi ya Mourinho.
Atkinson
aliwaita wote wawili na kuwadokezea kuwa endapo wataendelea na sakata lao la aibu kubwa uwanjani basi atawapeleka jukwaani.
Wenger
na Mourinho waliendelea kubadilishana matusi hata baada ya kutenganishwa karibu sehemu yote ya mchezo iliyosalia katika kipindi cha kwanza huku meneja msaidizi wa Chelsea Rui Faria na yule wa Arsenal Steve
Bould wakionekana kuingilia ugomvi wa wakubwa wao wa kazi.
Ndani ya uwanja matokeo haya yanakuwa ni kama aibu kubwa kwa Wenger, ambaye hayajawahi kumfunga Mourinho katika jumla ya michezo 11 iliyopita huku Eden Hazard akifunga goli kwa njia ya penati baada ya kufanyiwa madhambi na Laurent Koscielny ndani ya sanduku la hatari na kuwapa wenyeji Chelsea goli la kuongoza.
Bao la pili la washindi lilitiwa nyavuni na Diego Costa kunako dakika ya 78 ya mchezo likiwa ni goli la tisa kwa mshambuliaji huyo msimu huu wa ligi.
Mwamuzi Mark Atkinson akiwaita mabosi hao kufuatia tukio la aibu uwanjani na kutishia kuwaondoa katika eneo la ufundi na kuwapeleka jukwaani
Wenger alikasirishwa na rafu mbaya aliyofanyiwa mshambuliaji wake Alex Sanchez na Gary Cahill kunako dakika ya 20 ya mchezo.
No comments:
Post a Comment