Shirikisho la soka barani Afrika limesema linatambua juu ya mlipuko wa ugonjwa Ebola barani Afrika licha ya kugomea ombi la kuahirishwa kwa fainali za mataifa ya Afrika 2015.
Waandalizi wa mwezi Januari nchi ya Morocco italazimika kusubiri mpaka Jumamosi kuamua kama bado wanataka kuendelea kuandaa fainali hizo ama laa.
Hapo kabla walionyesha wasiwasi ya kuendelea na maandalizi hayo kufuatia kuripuka kwa ugonjwa huo kwa kasi kubwa katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Katibu mkuu wa Caf Hicham El Amrani amesema
"tunafahamu juu ya hali ya mambo ilivyo, na si hali nzuri kwa kila mmoja wetu.
"tunajua juu ya tahadhari inayopaswa kuchukuliwa na mataifa lakini ni muhimu kuongeza hofu.
Yafuatayo ni madhara tayari ya Ebola katika soka la AfrikA |
---|
Sierra Leone imesimamisha shughuli zote za soka |
Caf imezifungia Guinea, Liberia na Sierra Leone kuandaa michezo ya kimataifa |
Seychelles imeondoa mchezo wake wa kufuzu AFCON dhidi ya Sierra Leone |