Mshambukliaji wa simba Emmanuel okwi
amekanusha taarifa za kuwa yuko mboni kuelekea katika klabu ya Yanga akisema taarifa
hizo zilikuwa ni uzushi mtupu.
Okwi amesema ameshangazwa na taarifa
kuwa huenda akaelekea katika klabu hiyo yenye maskani yake katika makutano ya
mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es salaam.
Akiongea na Rockersports akiwa tayari
yuko jijini Dar es salaam amesema yeye hana mpango wowote wa kuelekea kucheza
soka katika klabu ya Yanga na kwamba bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake
ya Saimba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi.
Okwi amekanusha juu ya kukutana na
mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Abdalah Bin Kleb huko katika jiji la
Kampala nchini Uganda akisema taarifa hizo amezisikia alipofika jijini Dar es
salaam.
Kuhusu taarifa za majaribio yake
nchini Austria katika klabu ya fc Salzburg amesema yamekwenda vizuri na kilicho
mrudisha nyumbani Afrika ni kutokana na kupatwa na malaria ambayo alilazimika
kujitibia nchini Uganda.
Kuhusu hatma yake ya baadaye katika
soka amesema yeye ni mchezaji halali wa Simba na atakuwepo katika tamasha
maarufu la klabu hiyo maarufu kama Simba Day isipokuwa hatakuwepo uwanjani kwa
kuwa bado ana sumbuliwa na malaria.
Rockersports pia ilibahatika kuongea
na makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu ambaye amesema
wamefurahishwa na kuwasili kwa Okwi na kwamba atatambulishwa kwa wanachama na
wapenzi wa klabu hiyo kama itakavyokuwa kwa wachezaji wengine katika uwanja wa
Taifa kabla ya mchezo dhidi ya Nairobi City Stars ambao ni kuhitimisha sherehe
ya Simba Day.
akifeli majaribio ndio hivyo tena atakuwa amebakiza mwaka mmoja amba ikibaki miezi sita atakuwa huru kuzungumza na timu yoyote na kama muda huo ukimalizika atakapopata timu simba haitaambulia hata senti tano,habari ndiyo hiyo
ReplyDelete