Mkurugenzi wa TFF Sadi kawemba |
Kufuatia
tishio la chama cha soka Zanzibar ZFA kutaka kuziondoa timu zao katika michuano
ya BancABC sup8r inayoendelea hivi sasa, shirikisho la soka nchini TFF
limelazimika kumtuma mjumbe wake bwana Sadi Kawemba kuelekea visiwani huko kwa
ajili ya kutuliza hali hewa.
Kawemba
ambaye ni mkurugenzi wa mashindano TFF ameondoka hii leo kwa lengo la kukutana
na uongozi wa ZFA ambao atawaonyesha mchanganuo mzima wa mgawanyo wa fedha za
mdhamini BancABC kwa ajili ya michuano hiyo iliyozuka ghafla kwa shinikizo la
pesa nje ya kalenda ya mwaka ya matukio ya TFF.
Taarifa
iliyotolewa hii leo na TFF imesema kuwa BancABC imetoa shilingi milioni 880
kudhamini ligi hiyo ndogo inayoshirikisha jumla ya timu nane nne kutoka bara na
nne nyingine kutoka Zanzibar.
Hapo kabla
ligi hiyo ilikuwa ishirikishe vilabu vikubwa kwa kutumia timu zao za vikosi vya
kwanza na zilizo shika nafasi za juu katika ligi za msimu uliopita lakini mambo
yakaenda mrama ambapo vilabu vya Simba, Yanga na Azam kwa Tanzania Bara
vilikuwa vinastahili kushiriki kuonekana kugomea mpaka wapewe uwazi wa maslahi
gani wapata kwa kushiriki ligi hiyo ambayo iliibuka ghafla kinyume na ratiba ya
mwaka ya matukio ya TFF.
Hata hivyo baadaye
Simba ikakubali kushiriki lakini kwa kutumia timu ya vijana tofauti na Azam
ambao bila masharti wakaingiza timu yao wakati
ambapo mabingwa wa kombe la Kagame Yanga ikaamua kuitosa moja kwa moja ligi
hiyo.
Hatua ya TFF
kumtuma mjumbe wake Sadi Kawemba kwenda Zanzibar inaonekana ni kuajaribu kutuliza
hali ya hewa wakati ambapo ligi hiyo ndogo inaendelea na ZFA ikiwa tayari imeshaagiza timu zao kujiondoa.
Rockersports jana iliiongea na katibu wa ZFA Kassim Haji ambaye aliotoa sababu mbalimbali za kutaka kuziondoa timu zao kuwa ni pamoja kutokuwepo kwa mawasiliano ya baina ya TFF na ZFA kuhusu ligi hiyo ndogo ambayo ina sura ya muungano.
Jamabo la pili ni kuwa hawajui chochote kuhusu mapato ya ligi hiyo ambayo inashirikisha timu za idadi sawa toka kila upande .
Jambo lingine ni kuwa TFF kuwaambia kuwa watafadika na makusanyo ya mapato ya milangoni ilhali wao TFF wakijua kuwa makusanyo kwa upande wa Zanzibar si zaidi ya shilingi elfu hamsini wakati ligi hii imedhaminiwa kwa shilingi milioni 880.
Kassim Haji akaendele mbali zaidi akisema licha ya kuomba kukutana na katibu wa TFF kujadili kwa kina juu ya hayo bado katibu wa TFF Angetile Oseah hakuwa tayari kukutana naye zaidi ya kumtuma mkurugenzi wa mashindano Sadi Kawemba jambo ambalo wao kama ZFA ilionekana ni dharau toka kwa mtendaji huyo wa TFF.
Madai ya TFF ni kwamba hata wao ZFA walipo andaa michezo ya ujirani mwema walialikwa ili vilabu vya Bara kushiriki jambo ambalo hawakuhoji kiundani nini maslahi ya TFF katika ligi ile .
Hata hivyo Kasim haji amejibu kuwa walikubali michezo miwili ya nusu fainali na fainali kuchezwa bara na TFF ilichukua mapato ya michezo hiyo ambayo kimsingi yalikuwa ni makubwa kuliko michezo yote iliyochezwa Zanzibar katika hatua ya makundi.
Timu za Zanziba zinazo shiriki ligi hiyo ni Jamhuri, Zimamoto
Mtende
na Super Falcon wakati ambapo timu kutoka bara ni Simba,Azam, Mtibwa Sugar
na Polisi Moro.
No comments:
Post a Comment