Aliyekuwa kiungo wa timu ya Azam fc Ramadhani Chombo Lidondo amesema makataba alioingia na klabu yake ya zamani ya Simba ni mkataba halali kwa kuwa mkataba wa Azam na yeye ulimalizika tangu mwezi June.
Lidondo amesema Azam ilikuwa imempa muda wa kusubiri kumalizika kwa michuano ya Kagame ndipo aingie mkataba mpya na klabu hiyo jambo ambalo klabu hiyo ilishindwa kufanya hivyo mpaka kufikia siku ambayo ameingia mkataba na wekundu wa msimbazi.
Lidondo na Simba wamekubaliana kuwa pamoja kwa kipindi cha miaka miwili kwa mujibu wa makataba wao ambao uliingiwa rasmi juzi.
No comments:
Post a Comment