Mabingwa wa
soka Tanzania bara Simba kesho wanaelekea mkoani Arusha tayari kwa ajili
ya matayarisho ya kitimtimu cha ligi kuu Tanzania Bara kinachotarajiwa kuanza
kutimua vumbi mapema mwezi ujao.
Simba inaelekea
Arusha baada ya kumaliza tamasha lake la Simba Day hapo jana tamasha ambalo liliingia doa pale
walipokubali kipigo cha mabao 3-1 mbele ya Nairobi city stars ya nchini Kenya.
Afisa habari
wa simba Ezekiel Kamwaga ameiambia Rockersports kuwa watakuwa Arusha mpaka siku
ya mchezo wa ngao ya hisani august 25 ambapo watakuwa wakicheza dhidi ya
washindi wa pili wa ligi ya bara Azam fc.
Wakiwa mkoani Arusha tarehe 18 august Simba itacheza na AFC Leopards ya Kenya ukiwa ni mchezo pekee wa kujipima nguvu kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kujiwinda na mchezo wa ngao ya hisani agust 25 dhidi ya Azam fc.
Kumbuka ligi kuu ya soka Tanzania Bara imepangwa kuanza Septemba mosi.
No comments:
Post a Comment