Reds huenda wakauza haki ya kumiliki
jina la klabu
Mmiliki mkuu
wa Liverpool John W Henry amesema anafikiria kuuza haki inayotokana na jina la Anfield ili kuongeza pato la klabu
hiyo.
Henry pia
amewataka wakuu wa Premier League kuangalia juu ya sheria ya matumizi “Financial
Fair Play” akitoa lawama kwa wapinzani wa Liverpool kupuuza sheria za aina hiyo
za UEFA zilizotengenezwa kujaribu kuweka usawa katika kumbukumbu za vitabu.
Mmarekani
huyo ameweka wazi kuwa yeye na kundi maarufu la Fenway Sports wanaangalia zaidi soko la nje
kujaribu kusaidia kukuza kipato na kuweka nembo mpya katika nyumba mpya ya Liverpool katika historia ambayo huenda
ikawekwa katika kadi za wanachama.
amenukuliwa hayo
kupitia Tomkins Times.
"Hii
klabu inatakiwa kujiwezesha yenyewe kuongeza kipato chake lakini haitakuwa
rahisi"
"lakini
sitaki kuona hilo linafanyika katika kiwango cha kawaida kwa kipimo cha hapa
nyumbani bali kwa kiwango cha dunia.
"haki
itokanayo na jina Anfield inaweza ikaja
kama marafiki watakuwa wako sawa lakini bado hatuja shawishi juu ya hilo."
Henry amesema
Liverpool inataka kuwa na uwezo wa kujitegemea huku akikosoa vilabu ambavyo
vimefanya matumizi makubwa .
Manchester
City ilichapicha hasara ya pauni milioni £197 katika mwaka wa fedha wa 2010-11 wakati
ambapo Chelsea ikiwa imesha lipa zaidi ya pauni £60 kusajili wachezaji wapya
msimu huu.
UEFA inayo
nguvu ya kuviondoa vilabu ambavyo vimetangaza kupata hasara ya zaidi ya euro
milioni 45 ndani ya kipindi cha miaka mitatu kutokushiriki michuano ya ulaya na
Henry anaweka makazo kuwa hilo linaweza kutokea kweli na kuwataka wakubwa wa
Premier League kuchuakua hatua.
amenukuliwa
akisema
"Katika
siku za hivi karibuni nilisema nusu ya vilabu katika timu za vilabu vya ligi
kuu barani ulaya vinaingia katika hasara na asilimia 20 vinapoteza kabisa uwezo
wa kisheria kuendelea kusalia katika ligi.
"tuna
imani waendesha ligi wenyewe wanapaswa kusimamia sheria ambazo zinaoneka
kupuuzwa na vilabu ambazo pia ni sheria za UEFA, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa
linavifanya vilabu kusema kuwa kupoteza pesa ni jambo la kawaida na kuondoa
maana ya adhabu hiyo ."
Liverpool huko
nyuma ilikosolewa kwa kuafanya malipo ya ziada katika zoezi la uhamisho tangu FSG
kuchukua klabu hiyo mwaka 2010 ambapo karibu pauni milioni £130 zilitumika
lakini Henry ansema
"ni
wajibu wa LFC kuwekeza barabara kwa wachezaji ili klabu hiyo
isitetereke na kuwa “powerhouse."
Cristiano Ronaldo ana imani Kaka ataendelea
kuwepo Real Madrid
|
Cristiano Ronaldo |
Cristiano
Ronaldo ana imani kuwa Ricaldo Kaka ahataondoka Real Madrid msimu huu.
Kiungo huyo
raia wa Brazil bado ameendelea kuhusishwa na kutaka kuelekea AC Milan
ananukuliwa
Ronaldo akisema
"kuondoka
au kutokuondoka ni maamuzi yake lakini nadhanio atasalia hapa".
"kwa
upande wangu ni mchezaji mzuri sana duniani na wachezaji wote wazuri
wanastahili kuwepo hapa Real Madrid."
Nyota huyo
wa kimataifa wa Ureno kwasasa anaangalia mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Valencia
katika ligi ya Hispania La Liga na amesisitiza kuwa wanataka kuanza msimu
katika kiwango cha juu.
Madrid watakuwa
wenyeji wa Valencia katika mchezo utakao pigwa Santiago Bernabeu August 19.
Kagawa na Honda wamejumushwa katika
kikosi cha Japan kabla ya mchezo dhidi ya Venezuela
|
Kikosi cha timu ya taifa ya Japan |
Chama cha
soka cha Japan (JFA) hii leo kimetangaza majina ya wachezaji wake wa timu ya
taifa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Venezuela jumatano ijayo mjini Sapporo.
Nusu ya
wachezaji wa kikosi hicho cha wachezaji 22 players wanatokea katika ligi
mbalimbali barani Ulaya isipokuwa wachezaji 11 ndio wanaotokea katika timu za ligi
ya nyumbani J-League.
Yumo mchezaji
mpya wa Manchester United Shinji Kagawa na nyota wa CSKA Moscow Keisuke Honda pia
Ryo Miyaichi wa Arsenal lakini mlinzi Atsuto Uchida, Yuzo Kurisawa, na Yasuyuki
Konno wakiachwa lakini ni tangu walivyo achwa katika kikosi cha mwezi September
mwaka jana katika kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Iraq.
Japan watakuwa
wenyeji wa Venezuela kule Sapporo Dome August 15.
kikosi kamili
Magolikipa: Eiji Kawashima (Standard Liege),
Shunsaku Nishikawa (Sanfrecce Hiroshima), Shuichi Gonda (FC Tokyo)
Walinzi: Yuichi Komano (Jubilo Iwata), Maya
Yoshida (VVV), Daiki Iwamasa (Kashima Antlers), Masahiko Inoha (Vissel Kobe),
Yuto Nagatomo (Inter), Tomoaki Makino (Urawa Reds), Hiroku Mizumoto
(Sanfrecce), Gotoku Sakai (Stuttgart)
Viungo: Kengo Nakamura (Kawasaki Frontale),
Makoto Hasebe (Wolfsburg), Hajime Hosogai (Leverkusen), Keisuke Honda (CSKA
Moscow), Hideto Takahashi (FC Tokyo), Yasuhito Endo (Gamba Osaka)
Washambuliaji: Ryoichi Maeda (Jubilo), Shinji
Okazaki (Stuttgart), Kengo Fujimoto (Nagoya Grampus), Shinji Kagawa (Manchester
United), Mike Havenaar (Vitesse), Ryo Miyaichi (Arsenal)
Lahm na Podolski waondoshwa kikosini
Ujerumani dhidi ya Argentina
|
Kocha Joachim Low wa Ujerumani |
Kocha wa
timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amefanya uchaguzi wa wachezaji wake wa
kikosi cha timu ya taifa ambacho kina jumla ya wachezaji 19 ikiwa ni kwa ajili
ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Argentina mchezo ambao utapigwa August
15.
Nahodha Phiipp
Lahm ahatakuwepo kikosini kufuatia kuwa katika matayarisho ya kupata mtoto
ndani ya kipindi cha kambi ya timu hiyo wakati ambapo wakali wa Arsenal Lukas
Podolski na Per Mertesacker wakiwa katika matayarisho ya kuanza kwa msimu
mpyawa ligi ambapo klabu yao ya Arsenal itafungua msimu wa ligi ya uingereza
dhidi ya Sunderland August 18.
Low amenukuliwa kupitia mtandao wa chama cha
soka cha ujerumani akisema
“Philip
[Lahm] anataka kucheza lakini baada ya kuongea naye kwa njia ya simu nimeamua
kumuacha kwa ajili ya mambo binafsi ya kimaisha”.
mlinda
mlango wa Hoffenheim Tim Wiese naye amekatwa ikiwa sasa huenda ikawa ndio moja
kwa moja kutokana na sera ya Ujerumani kutaka kuwatumia zaidi vijana na katika
nafasi hiyo sasa ikiwa imemuangukia Manuel Neuer.
Toka Bayern
Munich Bastian Schweinsteiger na Mario Gomez hawajajumuishwa kufuatiwa
kusumbuliwa na majeraha na Low akimuingiza mshambuliaji mzoefu mmoja ambaye
yuko katika kiwango kizuri Miroslav Klose toka Lazio ya italia.
Ferguson alalamikia Arsenal
|
Alex Furguson |
Mkataba wa
mshambuliaji wa Arsenal Robie Van Persie kutoka nchini Uholanzi mwenye umri wa miaka 29, umebaki na mda wa miezi
11 na amekataa kuongezea muda wake akichezea kwenye uwanja wa Emirates.
Sir Alex
Ferguson ameiambia BBC kuwa "tumewasilisha ombi letu kwa Arsenal, lakini
wao wamekua wakijaribu kujadiliana na vilabu vingine huku sisi tukisubiri.
Sielewi kinachoendelea huko wala sijaweza kupata mawasiliano na viongozi wa
Arsenal.
Mara ya
kwanza kwa Ferguson kuonyesha nia ya klabu yake kumtaka Van Persie ilikua tareh
20 Julai, na haijafahamika kama wamezidisha kiwango cha fedha walichopendekeza
wakati huo.
Inaeleweka
kuwa Arsenal haipo tayari kuanza mazungumzo ya aina yoyote ikiwa upande mmoja
unapendekezo la fedha lililo chini ya pauni milioni 20 za Uingereza.
"sielewi
mawazo ya Arsenal kwa sababu hawajatoa ishara yoyote," Aliwambia wandishi
wa habari baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Barcelona mjini Gothenburg mnamo
siku ya Jumatano, iliyomalizka kwa 0-0 kabla ya Barca ishindwa kwa 2-0 kupitia
mikwaju ya peneti.
Ni vigumu
kuelewa jinsi Arsenal inavyoendesha biashara, alizidi kulalamika Ferguson. Sina
maelezo zaidi ya kuwafahamisha. Itabidi tuendelea kuwa na subira.
Robin Van
Persie kwa wakati huu yuko na kikosi cha Arsenal kwenye ziara ya Ujerumani
ambako watacheza mechi ya kirafiki. Meneja wa Arsenal, alisema hivi karibuni
kua atajitahidi kuona kua mshambuliaji wake bora anabaki kuichezea Arsenal.
Wakati huo
huo, Ferguson alikiri kua alipata kizunguzungu aliposikia kua shabaha yake ya
pili Lucas Moura amekubali kujiunga na klabu ya Ufaransa Paris St-Germain.
Mchezaji huyo aliyeiwakilisha Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki mjini
London, atatiunga na PSG mnamo mwezi Januari 2013 kwa mkataba wa miaka minne na
nusu kutoka Sao Paulo. Ferguson aliongeza kusema, PSG wamemsajili Thiago Silva
na Zlatan Ibramovic, huenda wametumia hadi pauni milioni 150 mwezi uliopita tu.
No comments:
Post a Comment