Katika kukamilisha hafla kubwa ya siku ya Simba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , klabu Simba imeshindwa kuwapa furaha mashabiki wake baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa timu Nairobi City Stars.
Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutangaza na kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao wa kimashindano kwa klabu hiyo kongwe nchini.
Simba iliwatambulisha wachezaji wake wote akiwemo Emmanuel Okwi ambaye katika siku za hivi karibuni alikuwa nchini Ausrtia katika klabu ya FC Saulburg kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka katika klabu hiyo ambapo taarifa zinasema mchezaji huo ameshindwa kufuzu.
Wengine waliotambulishwa ni pamoja na Mrisho Ngasa ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia klabu ya Azam.
wengine ni Ramadhani Chombo Lidondo aliyekuwa Azam, Ahmed Waziri ,Mbuyi twitte ,Abdalah Juma , Kanu Mbiyavanga Mussa Mude,Danny Mruanda na Paul Ngalema.
Hata hivyo katika mchezo wa leo Simba haikuonyesha soka la kuwafurahisha mashabiki wake mbali ya kuonekana kocha Molovan Circkovic akibalisha wachezaji wake kila mara ambao waliufanya mchezo huo kudorora zaidi huku wapinzani wao Nairobi City Stars kuonekana wakifanya vizuri hususani katika kipindi cha pili ambapo walifanikiwa kuandika mabao yao yote matatu.
Kimsingi kocha ana kazi ya kujua vema kikosi chake cha kwanza kwani kwani bado wachezaji wa Simba hawajafahamiana vema hasa sehemu ya kiungo ambapo kwa leo Mwinyi Kazimoto,Haruna Moshi,Amri Kiemba,Kanu Mbiyavanga kila mmoja kuonekana ana uwezo binafsi.
Hata hivyo ukiachana na mchezo huo kwa ujumla tamasha hilo limefana sana kwani mapema kulifanyika zoezi la kutoa misaada katika hospitali ya Mwananyamala, kisha michezo ya timu za wanawake katika uwanja wa Taifa ambapo ilitambulishwa timu ya Simba ya wanawake na hata tuzo mbalimbali kutolewa kwa wachezaji.
Shomari Kapombe amekuwa mchezaji mwenye nidhamu Emmanuel Okwi mchezaji bora msimu uliopita marehemu Patrick Mafisango akipewa tuzo maalum ambayo imetokana na mchango wake msimu uliopita na mzee Hamisi Kilomoni akipewa tuzo ya heshima.
No comments:
Post a Comment