KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 9, 2012

JULIO WACHEZAJI WANAKULA SANA WAKIWA MBEYA, APONGEZA KAMBI YA SERENGETI BOYZ MKOANI MBEYA.


 Kocha msaidizi wa timu ya vijana ya  wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boyz Jamhuri Kihwelu Julio amekipongeza chama cha soka cha mkoa wa Mbeya MRFA kwa kuandaa kambi ya timu hiyo ya vijana mkoani humo na kuwaandalia michezo kadhaa ya kujipima nguvu.
Akiongea na Rockersports akiwa mkoani humo Julio amesema kambi hiyo imewasaidi sana kiufundi kwani wachezaji wake mbali ya mazoezi mazuri wanayopata pia wamekuwa katika muda mzuri wa kupumzika.
Serengeti Boys inatarajia kucheza dhidi ya timu ya taifa ya vijana ya Misri mchezo ambao umepangwa kucheza Oktoba 14 mwaka huu ambao utapigwa nchini Tanzania kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Misri kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu. Mshindi baada ya mechi hizo mbili ataingia raundi ya tatu ambayo ndiyo ya mwisho kabla ya kwenda Morocco.

Julio amesema kambi yao ya mkoni Mbeya imekuwa nzuri kwani wamekuwa wakicheza na timu nzuri na ambazo zimekuwa zikiwapa mazoezi ya nguzu na kurekebisha makosa katika michezo mingine pia wachezaji wamekuwa wanakula chakula kingi jambo ambalo ni zuri kujenga afya na nguvu ya mchezaji.

Amevitaka vyama vingine vya soka vya mikoa kuiga mfano wa viongozi wa soka wa mkoa wa Mbeya ambao wamekuwa wakiwapa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapangia michezo mizuri huku pongezi kubwa akizipeleka kwa mwenyekiti wa MRFA Selemani Ayubu pamoja na viongozi wengine wa MRFA.

Kikosi hicho cha Serengeti kimecheza michezo miwili ikiwa ni pamoja na Tanzania Prisons pamoja na Mbozi United lakini pia wanatarajia jumatatu kucheza dhidi ya Mbeya City kabla ya kuelekea Tukuyu mkoani humo kucheza mchezo mwingine Alhamisi kwa mchezo mwingine kabla ya kurejea jijini Dar es salaam. 

Katika hatua nyingine timu hiyo imefungwa bao 1-0 na Mbozi United katika mfululizo wa michezo yao ya kujipima nguvu mchezo uliopigwa jumapili hii.
BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment