KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 9, 2012

KIMATAIFA:Giggs: Usajili wa Van Persie,Manchester United imesajili mchezaji wa kiwango cha dunia,Didier Drogba anasema atasalia China na kuisaidia Ivory Coast kutwaa taji la Africa Cup na Fellaini anafikiria kuondoka Everton.


Giggs: Usajili wa Van Persie,Manchester United imesajili mchezaji wa kiwango cha dunia
 Ryan Giggs ana matumaini kuwa usajili wa Robin Van Perise , Manchester United imesajili "world-class star" na kwamba Robin van Persie ataisaidia sana United kuelekea katika taji la 20 msimu huu.
Wakati  United ikipoteza taji kwa majirani zao Manchester City kwa utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa  msimu uliopita, mwingereza huyo mwenye asili ya Wells anaamini Van Persie amekwenda kuepeleka mazuri baada ya kuifungia Asernal jumla ya mabao 30 katika msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo aliyeigharimu United jumla ya pauni za kingereza milioni 22  anaonekana kuwa ni katika mpango wa meneja Sir Alex Ferguson  wa kusajili vijana wenye kiwango.
Tayari Van Persie ameshaifungia united jumla ya mabao manne jambo ambalo limemfanya  Giggs kuamini kuwa United imelamba dume.
Amenukuliwa na Sky Sports News akisema
"mabao ambayo Van Persie alichoonyesha kwa ujumla ni wazi kuwa ni mchezaji wa mchezaji wa kiwango cha dunia.
"sera ya meneja kwa kipindi cha miaka 10 mpaka 15 ni kusajili vijana wachanga na kuwaendeleza yokuwa kwa Cristiano [Ronaldo], na Wayne [Rooney].
"lakini  Robin  tayari amesha dhihirisha kuwa tayari katika kiwango cha dunia . ameonyesha hilo katika michezo michache na nataraji mengi yanakuja."

 Didier Drogba anasema atasalia China na kuisaidia Ivory Coast kutwaa taji la Africa Cup
 Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba amesema kuwa ataendelea kusalia nchini china na akiwa huko amedhamiria kuisaidia nchi yake ya Ivory Coast kushinda taji la Africa Cup mwakani na kucheza soka la kiushindani.
Mshambuliaji huyo wa sasa wa Shanghai Shenhua ndiye aliyefunga goli la penati katika mchezo wa ushindi wa mabao 4-2 jana mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Senegal mjini Abidjan.
Amesema kuwa kwasasa anaweka mawazo yake katika hilo na kuwataka mashabiki wa soka kukaa mkao wa  kula na kusisitiza kuwa si tu yuko barani Asia kucheza soka la ngazi ya klabu l,itakalo mpeleka kustaafu , bali pia kutoa msaada kwa taifa lake.
Amenukuliwa na gazeti la L‘Equipe akisema
"kwa kuelekea katika fainali za mataifa ya Afrika 2013 , nitafanya kila kitu kuendelea kuwa na kiwango cha kiushindani nikiwa nchini china. Msiwe na wasiwasi,"
Wakati matokeo ya mchezo yakisomeka 2-2, Drogba droba alifanikiwa kuandika bao la tatu kabla ya Max Gradel kuongeza kika tano mpira kumalizika.
 Itakumbukwa Drogba alikuwa katika mwaka wa kupanda na kushuka ambapo alikosa penati katika mchezo ambao Ivory Coast ilifungwa na Zambia mchezo wa fainali mwezi  February, lakini aliibuka kuwa shujaa katika maguu 12 ya penati, mchezo wa vilabu bingwa barani ulaya wakati huo akiwa na klabu yake ya zamani ya Chelsea dhidi ya  Bayern Munich miezi mitatu iliyopita.

 Fellaini anafikiria kuondoka Everton 

Kiungo wa Everton Marouane Fellaini ametanabaisha kuwa yuko katika mtazamol wa kuondoka katika klabu yake msimu ujao wa majira ya kiangazi.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga  Goodison Park akitokea Standard Liege ya Ubelgiji September 2008, tayari ameshafun ga jumla ya mabao mawili katika kikosik cha meneja David Moyes msimu huu.
Fellaini alisaini kuichezea klabu yake ya Everton mkataba wa miaka mitano November 2011 lakini mchezaji hnuyo wa kimataifa wa Ubelgiji amesisitiza kuwa huu utakuwa ni msimu wake wa mwisho ndani ya klabu hiyo.
Amenukuliwa akisema
"sasa naanza msimu wangu wa tano na Everton, huu utakuwa msimu wangu wa mwisho kimeona kila kitu mwezi januari au mwisho wa msimu nitakuwa naangalia klabu nyingine."
 Mapema mwezi mwezi huu wa September, Everton ilikuwa imependekeza kumsajili kwa mkopo kiundo wa  Club Brugge ,Vadis Odjidja-Ofoe lakini mpango huo ulishindwa kuthibitishwa na FIFA .

No comments:

Post a Comment