KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 10, 2012

TENGA AWATAKA WAAMUZI KUTUMIA VIZURI SEMINA YA FIFA YA FUTURO III

     








 










Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Leordinga Tenga amewataka waamuzi wa mpira wa miguu barani Afrika kufuata kutafsiri vizuri sheria za mpira wa miguu ili kuleta maendeleo ya mchezo huo barani humu.
Kauli hiyo ameitoa hii katika hotuba yake ya ufunguzi wa kozi ya wakufunzi wa waamuzi (Futuro III Refereeing Course) ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambayo imeanza leo katika hotel ya Holiday inn jijini Dar es Salaam.
 
Jumla ya washiriki katika kozi hiyo itakayoanza saa 3 asubuhi kwenye hoteli ya Holiday Inn ambao wanatoka katika nchi 21 za Afrika ni 69. Kozi hiyo inayotarajiwa kumalizika Septemba 22 mwaka huu inafanyika katika maeneo mawili ya ufundi (technical) na utimamu wa mwili (fitness).
 
Nchi washiriki ni Afrika Kusini, Botswana, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Liberia, Malawi, Mauritius, Namibia, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
 
Washiriki kutoka Tanzania kwenye kozi hiyo ni Joan Minja, Leslie Liunda na Soud Abdi (technical) na Riziki Majalla (fitness).
 
Baadhi ya wakufunzi wa kozi hiyo wanaotoka FIFA na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Carlos Henriques anatoka Afrika Kusini, Fernando Gracia (Hispania), Steve Bennett (Uingereza), Tarek Bouchamaoui (Tunisia), James Sekajugo (Uganda), Bester Kalombo (Malawi), Felix Tangawarima (Zimbabwe) na An-Yan Lim Kee Chong (Mauritius).
 
Tenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na mjumbe wa Kamati ya Vyama (Associations Committee) ya FIFA amesema ni vizuri mafunzo hayo yakatumiwa vizuri sio tu kutoa elimu kwa waamuzi juu ya mabadiliko katika sheria za soka bali pia ni kuleta mtazamo mpya katika tasnia ya waamuzi ulimwenguni.
 

No comments:

Post a Comment