KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 10, 2012

RIPOTI YA VAZI LA TAIFA YAWASILISHWA KWA WAZIRI WA HABARI FENERA LEO , TAZAMA AINA YA VITAMBAA VILIVYOWASILISHWA.

      
 








 




HIVI NI BAADHI YA VITAMBAA VILIVYO WASILISHWA KWA WAZIRI FENERA MKANGARA TOKA NDANI YA RIPOTI YA KAMATI YA VAZI LA TAIFA




Waziri fenera na mama Joyce Mhavile


 Mchakato wa kuelekea kupata vazi la taifa umefikia hatua za mwisho mwisho ambapo hii leo ripoti ya mchakato imewasilishwa kwa waziri wa habari utamaduni na michezo Dr Fenera Mukangara akiwa pamoja na naibu wake Amos Makalla.

Uwasilishaji wa ripoti hiyo umefanywa na katibu wa kamati ya vazi la taifa Angela Ngowi Katibu aliye ambatana na wajumbe wa kamati Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali na Ndesambuka Merinyo.
Akiongea na waandishi wa habari waziri Dr Fenera ameipongeza kamati hiyo kwa kazi waliyo ifanya ambapo kamati hiyo hiyo ilifanikiwa kupita katika kanda mbalimbali ili kukusanya maoni ya wadau na wananchi kwa ujumla katika kufikia malengo yake.
 
Dr Fenera amesema anatarajia mpaka kufikia mwezi wa kumi kuna uwezekano mkubwa wa vazi hilo la taifa likawa limekwisha kupatikana na hivyo kuwataka Tanzania kulikubali vazi hilo na kujivunia ubunifu mkubwa uliofanywa na wanakamati ambao ndani yake kuna wabunifu wa mavazi wa kitanzania.

Ripoti hiyo imewasilishwa na katibu wa kamati hiyo Angela Ngowi aliyeambatana na baadhi ya wajumbe wake Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali na Ndesambuka Merinyo.
 
Pamoja na kuwasilisha ripoti yao pia walitumia nafasi hiyo kuonyesha baadhi ya ubunifu wa vitambaa  ambavyo vimebuniwa na wabunifu mbalimbali ambavyo vimewekwa nakshi zinazotokana na rasilimali za kitanzania.

No comments:

Post a Comment