KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 12, 2012

YANGA SAFARINI MBEYA ASUBUHI KESHO, KUANZA LIGI DHIDI YA PRISONS. SEINTFIET ATAJA SILAHA ZA MBEYA.



KOCHA Mkuu wa Yanga,  Tom Saintfiet ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya ufunguzi ya michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Prisons itakayochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam hii leo, Saintfiet amesema ameteua wachezaji hao kutokana na mazingira ya mechi hiyo na pia uwezo waliouonyesha katika mechi za hivi karibuni za kirafiki na michuano ya Kombe la Kagame.

Amewataja wachezaji wanaotarajiwa kuondoka kesho asubuhi kwenda Mbeya kuwa ni walinda mlango Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Shadrack Nsajigwa, Juma abdul, Godfrey Taita, Mbuyu Twite, Kevin Yondan,  Nadir Haroub ‘Cannavaro’, David Luhende, Oscar Joshua na Stefano Mwasyika.

Viungo kuwa ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Haruna Niyonzima, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Nizar Khalfan, Shamte Ally na Simon Msuva wakati washambuliaji ni Jerry Tegete, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza.

Wachezaji ambao hawatakuwepo safarini Mbeya kwa  ajili ya mechi hiyo kuwa ni kipa Said Mohamed, Ladislaus Mbogo, Job Ibrahim, Juma Seif ‘Kijiko’, Salum Telela, Omega Seme, Nurdin Bakari, Idrisa Assega na Issa Ngao wa Yanga B, ambaye anakomazwa kikosi cha kwanza.

Pia kocha huyo amesema mchezo wao dhidi ya Prisons utakuwa mgumu kwa vile wapinzani wao watakuwa wakicheza kwenye uwanja wa nyumbani na mbele ya mashabiki wao, hivyo amejipanga vyema kukabiliana nao ili aweze kutimiza lengo la kuibuka na ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo

No comments:

Post a Comment