KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, September 13, 2012

KIMATAIFA:Iniesta kukosa michezo mitatu, Meireles arudi darajani unajua kasema nini?, Casillas anasema anataka kukaa miaka minane zaidi Madrid na Brazil kucheza na England kuadhimisha miaka 150 ya kuzaliwa kwa chama cha soka cha England FA.


Iniesta kukosa michezo mitatu
 Nyota wawili wa kimataifa wa Hispania Andres Iniesta na Jordi Alba wamerejea katika vilabu vya kutoka katika majukumu ya kimataifa wakiwa na majeraha na ugonjwa licha licha ya kumaliza dakika 90 katika mchezo wao wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Georgia jumanne iliyopita.
Imeelezwa kuwa Iniesta alipatwa na matatizo ya msuli katika mguu wake wa kulia na taarifa za madaktari wa klabu yao ya Barcelona zimethibitisha kuwa atakuwa nje ya uwanja ndani ya kipindi cha kuanzia siku 10 mpaka 15.
Kiungo huyo anatazamiwa kurejea dimbani katika michezo wa ligi ya Hispania maarifu kama ‘La Liga’ dhidi ya Getafe na mchezo mwingine dhidi ya Granada katika uwanja wa nyumbani Camp Nou lakini pia katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Spartak Moscow Jumatano ijayo.
Kwa upande wa Jordi Alba kuna wasiwasi wa kutokuonekana dimbani katika mchezo dhidi ya Getafe lakini huenda akawepo katika jiji la Madrid kama hatawekwa benchi.

Wakati hayo yakiwa hivyo Carlos Puyol amebandika picha yake katika ukurasa wa ‘Twitter sporting’ akionekana kuvaa kitu kama kinyago kuzuia jeraha lake la taya ambalo limekuwa likimsumbua na amekuwa akiendelea kufanyiwa matibabu.

Pazzini ataka AC Milan kukomaa na ushindi mnene
 Mshambuliaji mpya wa AC Milan Giampaolo Pazzini ametaka wachezaji wenzake kuendelea kukaza uzi uleule walioanza nao katika mchezo wa pili wa ligi kwenda nao msimu mzima kama kweli wanataka kupata mafanikio msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia alifunga mabao matatu ‘hat-trick’ katika mchezo dhidi ya Bologna ukiwa ni mchezo wake wa pili tangu ajiunge na Milan na anataka kikosi chake kujiweka katika nafasi nzuri katika kipindi hiki cha mapumziko ambacho nchi mbalimbali ziko katika michezo ya kimataifa.
Amenukuliwa na 'Milan channel' akisema
“Milan lazima kila mara iwe imeweka dhamira ya ushindi na tunatakiwa kuwa na uwezo wa kufunga mabao mengi".
"jumamosi tunakabiliana na Atalanta tunapaswa kimchezo kuwa katika asilimia 100".

Milan kwasasa iko katika nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Italia ‘Serie A’ kufuatika kushinda mchezo mmoja na kufungwa mmoja baada ya michezo miwili waliyokwisha kucheza tangu kuanza kwa ligi ya soka ya Italia.
  
Bentley: Bado naweza kuichezea England
 Winga wa Tottenham David Bentley amedai kuwa bado ana kiwango kizuri cha kuitumikia timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama Simba watatu, kauli ambayo imekuja kufuatia kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya ligi kuu ya Urusi  ya FC Rostov.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 28-ameelekea huko baada ya taarifa kusema kuwa ameshindwa kulinda kiwango chake White Hart Lane baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni €19 akitokea Blackburn Rovers mwaka 2008.

Winga huyo ameichezea Spurs michezo 48 ambapo katika michezo yote hiyo amefanikiwa kuzifumania nyavu mara tatu tu kabla ya kupelekwa kwa mkopo katika vilabu vya Birmingham City na West Ham ambako pia bado alishindwa kuonyesha uwezo.
Bentley alikuwa nje ya uwanja kwa miezi sita kufuatia kuwa na majeraha kule Upton Park, baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu, hata hivyo alitarajiwa kurejea katika fomu akiwa Tottenham baada ya kuwasili kwa Andre Villas-Boas, jambo ambalo pia aligonga mwamba.
Kinda huyo wa zamani wa  Arsenal ambaye kwa mara ya mwisho kuitumikia timu ya taifa lake la Uingereza ilikuwa ni mwaka 2008, anaamini kuwa bado anaweza kuichezea timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuachwa katika uteuzi wa hivi karibuni wa meneja wa timu ya Taifa Roy Hodgson.

“nilidhani meneja mpya angenipa nafasi, lakini inaonekana tayari kuna maji mengi chini ya daraja"
 
Meireles:Nilikuwa na wakati mzuri sana Chelsea nitaikumbuka sana klabu hii
 Raul Meireles amerejea katika viunga vya uwanja wake wa zamani wa klabu ya Chelsea vya Cobham hapo jana na kusema alikuwa katika kipindi kizuri cha maisha yake alipokuwa hapo kabla ya kuondoka na kujiunga na klabu yake mpya ya Fenerbahce.
Kiungo huyo alipokuwa katika kipindi cha utumishi wake wa miezi 12 Stanford Bridge, aliicheza Chelsea jumla ya michezo 48 ambapo alifanikiwa kushinda mataji ya mawili ya FA na ligi ya mabingwa ulaya
Kiungo huyo alikosekana katika mchezo wa fainali ya mabingwa kufuatia kupewa kadi nyekundu kule Camp Nou katika mchezo wa nusu fainali ya pili lakini bado alipata medali , ambayo kwake imekuwa ni fahari ya maisha yake ndani ya Stanford Bridge maeneo ya London ya kaskazini.

Amenukuliwa kupitia mtandao wa Chelsea akisema
"nimekuja kuwaaga marafiki zangu na kwa kweli nitaikumbuka klabu hii, mashabiki wake na jiji pia"

"kuna watu wazuri hapa ambao walinipa nguvu na wanasaidia kila mtu , hivyo nimekuja kuwaaga wote."
Meireles alijiungana Chelsea kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni  €15 akitokea Liverpool.

Casillas anasema anataka kukaa miaka minane zaidi  Madrid
 Mlinda mlango wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Iker Casillas amethibitisha kuwa mpango wake ni kuendelea kusalia katika klabu yake hiyo na kumalizia soka yake hapo, klabu ambayo alijiunga nayo akitokea kituo cha kukuza vijana cha Castilla.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 31 alianza kuidakia klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 18 na katika maadhimisho yake ya kuwepo katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 13, amenukuliwa akisema hana mpango wa kuondoka mpaka atakapo staafu kucheza soka.

“Ndoto yangu itakuwa kweli kama nitamalizia soka langu hapa".
"nilikuwa na ndoto ya kuichezea klabu hii tangu nikiwa na umri wa miaka minane , muda unakwenda haraka lakini nafurahia sana kile ambacho Real Madrid inanipatia na kile ambacho mimi pia nakitoa katika klabu."

Tangu ajiunge na Madrid , Casillas amekusanya mataji mbalimbali yakiwemo mataji mawili ya ligi ya mabingwa ulaya , mawili ya Intercontinental Cups,matano ya ligi, moja la  Copa del Rey, moja la European Super Cup na matatu ya Spanish Supercopas.
Pia ameshinda mataji ya kombe la dunia na kombe la mataifa ya Ulaya akiwa na timu ya taifa ya Hispania.

Ameendelea kusema kuwa
"miaka 13 imekwenda lakini tegemea mengi mazuri toka kwangu,".
"mkataba wangu unamalizika mpakara nitakapo kuwa na umri wa miaka 36, na ndoto yangu ni kustaafu nitakapo fikisha umri wa miaka 39”

Brazil kucheza na England kuadhimisha miaka 150 ya kuzaliwa kwa chama cha soka cha England FA.
Timu ya taifa ya Uingereza inatarajia kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Brazil katika uwanja wa Wembley ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki kuadhimisha miaka 150 ya chama cha soka cha Uingereza FA.
FA imetangaza kuwa mabingwa mara tano wa kombe la dunia watacheza na kikosi cha meneja Roy Hodgson Jumatano ya February 6 mwakani , pia kucheza na Brazil katika mchezo wa pili wa marudiano katika kipindi cha kiangazi.
Mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Ireland, umepangwa kuchezwa katika dimba jipya la Wembley, May 29, wakati ambapo jirani Scotland wakipangiwa kucheza mwezi August.

No comments:

Post a Comment